WANANCHI wameiomba Serikali kumchunguza mfanyabiashara maarufu raia wa China anayejihusisha zaidi na uagizaji nguo za mitumba na viatu kutoka nje ya nchi.

Wananchi hao waliyasema hayo walipozungumza na Morningstar Post katika ofisi zake zilizopo jengo la UMATI Barabara ya samora jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Wananchi hao ambao hawakupenda kutaja majina yao mtandaoni walisema mchina huyo ambaye jina lake tunalifadhi kwa sasa amekuwa akifungua makampuni kwa kutumia majina ya watanzania na kukwepa kulipa kodi mbalimbali kwa muda mrefu.

Walitoa mfano kampuni ya Dingguagua Investment inafanya biashara zake maeneo ya Keko Mwanga, wilaya ya Temeke, lakini hakuna leseni ya biashara.

Wakaongeza wamekuwa hawatoi risiti halali baadhi ya wateja wakidai risiti wanapewa lisiti ya duka lililopo Ilala na hivyo kuikosesha Manispaa ya Temeke mapato zaidi yanayotokana na leseni ya ghala na mauzo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa tovuti hii, imebaini licha ya kampuni hiyo kuwa na jina la kichina, TIN yake inasoma jina la Kitanzania la Bw. Manase.

Morningstar Post ilimtafuta mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw jong, kupata ufafanuzi wa tuhuma hizi kwa njia ya simu, alikiri yeye ni muhusika na aliomba mwandishi wa habari hizi kuongea na mhasibu wake anayeitwa Angel Swai.

Kwa upande wake bi Angel alikiri kuwa hawana mashine ya EFD na leseni ya biashara ya Temeke, na wanatumia mashine ya EFD ya Ilala ambayo pia imeharibika iko kwenye matengenezo.

Morningstar Post walimtafuta msemaji wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Bw. Richard Kayombo simu zake zote zilikuwa hazipokelewi.

Hata hivyo juhudi zinaendelea kumtafuta ili tupate ufafanuzi wa tuhuma hizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *