Taarifa Kata ya Buguruni
Madereva wa magari makubwa wametakiwa kulinda mitaa wanayoishi kama vile wanavyolinda usukani wa magari yao barabarani.
Wito huo umetolewa na Inspekta wa Jeshi la Polisi Nchini, wakati alipowatembelea waendesha maroli kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa ulinzi shirikishi.
“Mnamo tarehe 12/09/2024 majira ya saa 16:00hrs huko Buguruni Madenge A/INSP HADINANI aliwatembelea Waendesha malori na kuwapa elimu kuwa waweze kulinda mitaa Yao kama wanavyolinda usukani wakati wanaendesha wasiweze kusababisha ajali” inasema taarifa kutoka kata ya Buguruni.
Alisema inspekta Hadinani kuwa dereva mara nyingi huwa makini kabla ya kuendesha gari ikiwemo kukagua chombo chake kuanzia tairi mpaka vifaa vingine.
Pia aliwaeleza waweze kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu pindi wanapoitwa kubeba mali ya wizi.
Aidha, aliwakumbushia ulinzi jirani ambao sio nyumbani kwake tu bali hata nyumbani ya jirani ukitaka kutoka inabidi mutaarifiane ili kulinda nyumba zenu Ili hata ukisikia nyundo kwa jirani ujue sio mwenye nyumba bali ni mhalifu.
Inspekta Hadinani alihitimisha kwa kuwambushia madereva kufuata sheria za barabarani Ili kuepuka ajali zisizo za lazima.