Asali hii pamoja na umuhimu wake kwa matumizi ya watu, imewekwa kwenye chupa za pombe. Wajasiriamali wangeweza kubuni viifungashio vyao bidhaa ingekuwa bora yenye thamani zaidi.

Na Mohammed Ussi

WAJASIRIAMALI wadogo hapa nchini wameshauriwa kujifunza tabia ya kulinda bidhaa za wafanyabiashara wengine kwa kuongeza ubununifu wa kutengeneza vifungashio vya kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Habari dhidi ya Umasilkini Tanzania (MeCAP)) Bw. Mdoe Kiligo ameyasema hayo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Amesema kwamba matumizi ya hovyo ya vifungashio vya bidhaa zinazotengenezwa na Wajasirimali wadogo wakati mwingine yanavuruga soko lao wenyewe lakini pia kuharibu heshima ya vifungashio vya wafanyabiashara wengine.
“Sasa hivi imekuwa jambo la kawaida kuona mtu anazalisha bidhaa yake, lakini anatumia kifungashio cha kampuni nyingine. Tena bila aibu anashindwa hata kuomdoa nembo ya kampuni ile anayotumia kifungashio chake”, amesema Mdoe na kuongeza:
“Jambo hili ni baya na halimsaidii mhusika badala yake linaweza kumwingiza matatani ikiwa mwenye kifungashio chake ataamua kuchukua hatua za kisheria”.
Ametoa mfano wa wauza maziwa,
juisi ya miwa au matunda mengine mitaani ambao wamekuwa wakitumia chupa za kampuni za maji au soda, ambazo amesema licha ya usalama wake wa kiafya in 9⁹ ofkuwa mdogo, lakini haziwakilishi uhalisia wa kile kinachouzwa ndani yake.
“Nyingi kati ya chupa hizi zinaokotwa mitaani na hazioshwi katika kiwango kinachotakiwa. Walaji nao kwa bahati mbaya sana wamekuwa wakitumia juisi hizi bila kuzingatia usalama wa afya zao.”, amesema.
Anetoa mfano mwingine kuwa ni ule wa matumizi ya Tomato Sauce ambapo amesema kuwa wauza chipsi wengi, wamekuwa wakijaza tomato sauce inayotengezwa mitaani chini ya viwango kwenye chupa za kampuni nyingine.
“Kibiashara jambo hili linawaumiza wafanyabiashara ambao vifungashio vyao vinatumika wakati bidhaa iliyomo ndani ni duni. Walaji wanajua kabisa ubora wa kila kampuni, wakila chipsi ambazo tomato inayotumika kuongeza ladha ni feki, wanaanza kuwa na mashaka na ubora wa kampuni hiyo” amesema Mkurugenzi huyo.
“Angalia hata ukitembea tu mitaani utakuta wauza asali wengine wameweka asali kwenye chupa za pombe au kampuni za maji. Kwanini wasitengeneze vifungashio vyao na kuweka namba zao za simu ili kuwavutia wateja zaidi?” amehoji.
Amesema ili kuondokana na umasikini wajasiriamali wana mchango wao mkubwa, lakini lazima wawe wabunifu na wafanye shughuli zao kisasa zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *