Mhe Yahya Ally Mhata, Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu
Na Mwandishi Wetu
Taarifa ya Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, Mhe. Yahya Ally Mhata, kulalamikiwa na wakazi wa jimbo hilo, kushindwa kuwatembelea kushughulikia changamoto zao, imezua taharuki kwenye ofisi ya mbunge huyo.
Morningstar POST iliandika taarifa za baadhi ya wakazi wa jimbo la Nanyumbu, wakidai kuwa mbunge wao hatembelei jimboni kujua matatizo ya watu na anathamini sana watu wenye uwezo.
Aidha, Morningstar POST imefanya utafiti kuwa mbunge huyo kwa muda mrefu hajawahi kutembelea jimboni kwenye vijiji kama vile,
Maneme, Makanya, Nanyumbu. Kilimanihewa Ngalinje, Nachura, Namarupi, Mwambani. Masuguru-Lukwika. Chipuputa-Namasogo, Mkohora, Matihu Sengenya Mara, Masyalele, Kisimatuli.
Nanyumbu ina vijiji 93 lakini matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), 176 maana kuna vijiji vina matawi zaidi ya moja kutokana umbali wa kutoka kjijini hadi tawi.
Mbunge huyo analalamikiwa kushindwa kufika kwenye vijiji, ukizingatia hayo matawi yapo mbali na kijiji lakini mengine ni makubwa yana hadhi ya kijiji na hajapita.
Akijibu taarifa hizo kwenye ma-group ya whatsapp mtandaoni, mpambe wa mbunge huyo, mtu aliyejiita Katibu wa Ofisi ya Mbunge huyo ambaye hakutaja jina lake,
Alisema kuwa taarifa hiyo inamlengwa wa kisiasa na kudai kuwa mwandishi wa habari aliyeandika taarifa hizi sio mwana taaluma kwa kuandika habari za malalamiko ya wakazi wa jimbo la mbunge huyo.
“Ofisi ya Mhe YAHYA ALLY MHATA Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu imeona taarifa kupitia mtandao wa kijamii (WhatsApp) ikiwa na kichwa cha habari ” WAKAZI NAYUMBU WALIA NA MBUNGE WAO ” akimaanisha wakazi wa Nanyumbu.” inasema taarifa yake mpambe huyo.
Pia mpambe huyo anamwiita mwandishi wa taarifa hiyo kuwa ni mwandishi uchwara, alisema kuwa ofisi ya mbunge huyo inakanusha taarifa hiyo.
“Kwani hakuna Jambo hata moja sahihi lililoelezwa na mwandishi huyo pia kuna mashaka na taaluma ya mwandishi huyo kwani mwandishi wa habari professional hawezi kuripoti taarifa ambayo hajaifanyia tafiti hata kama atakua anatumika na wanasiasa walioanza kuaga mapambano mapema na kutumia njia dhaifu” alisema mpambe huyo kwa kebehi.
Aidha alimtaka mwandishi wa habari hizi kufanya utafiti wa vijiji ambavyo mbuge hajawahi kufika jambo ambalo mwandishi ameshafanya na kuwasiliana na Mwenyekiti wa CCM pamoja Mbunge ambao wahakuweza kukanusha taarifa hiyo.
Hata hivyo Morningstar POST inaendelea kumtafuta mbunge wa jimbo hilo kwenye simu yake ya mkononi ili kuzungumzia suala hilo la wakazi wa jimbo lake bila mafanikio mara kadhaa.