BBC

Donald Trump “anaendelea vyema” na anawashukuru maafisa wa kutekeleza sheria, kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya nje ya Kamati ya Kitaifa ya Republican (RNC).

Inasema “anatarajia kuungana nanyi nyote huko Milwaukee tunapoendelea na kongamano letu la kumteua kuhudumu kama rais wa 47 wa Marekani. Akiwa mteule wa chama chetu… [ataendelea] kushiriki maono yake ya Make America Great Again,” taarifa ya kampeni ya Trump na RNC imeeleza.

Trump aliwashukuru maafisa wa kutekeleza sheria na Huduma ya Siri kwa “majibu yao ya haraka”.

“Kikubwa zaidi naomba nitoe salamu za rambirambi kwa familia ya mtu aliyekuwa kwenye mkutano wa hadhara aliyeuawa, na pia kwa familia ya mtu mwingine aliyejeruhiwa vibaya, ni jambo la ajabu kuwa kitendo cha aina hii kinaweza kutokea katika nchi yetu, ” alisema.

“Hakuna kinachojulikana kwa wakati huu kuhusu mpiga risasi ambaye sasa amekufa. Nilipigwa risasi na kupenya sehemu ya juu ya sikio langu la kulia. Nilijua mara moja kuwa kuna kitu kibaya kwa kuwa nilisikia sauti ya kishindo, milio na risasi. mara akahisi risasi ikipasua kwenye ngozi.

“Kutokwa na damu nyingi kulitokea, kwa hivyo nikagundua ni nini kilikuwa kinatokea. Mungu Ibariki Marekani!”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *