Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroad Mohamed Besta
NA MWANDISHI WETU
Wakati Waziri wa ujenzi akionesha nia ya kuwalinda wakandarasi wa ndani, baadhi yao wamekuwa wakipuuza kufuata sheria zinazosimamia ujenzi hapa nchini.
Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa aliagiza kufuatiliwa kwa makandarasi wa nje ambao wanafanya miradi ya ujenzi chini ya viwango na kutaka wakandarasi wa ndani kupewa uwezo kusimamia miradi mikubwa.
Aidha, Wakala wa Barabara Nchni Tanroad imesema matumizi ya maudhui ya ndani yataongeza ukuwaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Maudhui ya ndani yanarejea matumizi ya makampuni ya ndani, nyenzo zinazopatikana nchini, taaluma binafsi katika kuendeleza miradi ya ujenzi nchini.
Wakati serikali inafanya jitiada za kuimarisha makampuni ya ndani ya ujenzi, baadhi ya wakandarasi wa ndani ndio wanaongoza katika kukiuka sheria zinazosimamia ujenzi hapa nchini.
Uchunguzi umefanywwa na Morningstar Post umebaini kuwa miradi mingi inayofanywa na makampuni ya ujenzi ya ndani ndio inaogoza kukiuka sheria za ujenzi.
Kama vile kusajili miradi kwenye mamlaka husiki, wakandarasi kuuza mabango na miradi mingi inasimamiwa na watu wasio tambulika na mamlaka husika.
Katika miradi mingi ya ujenzi iliyotembelewa jijini Dar es Salaam kumekuwa na mapungufu mengi ya kanuni na sheria zinazosimamia ujenzi.
Baadhi ya wakandarasi wa ndani wanashindwa kusimamia wafanyakazi wao kuwa na vifaaa vya kazi kwa usalama wa wafanyakazi.