Bw. Cyril Ramaphosa Rais ajaye wa Afrika Kusini.
BBC
Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance John Steenhuisen, amethibitisha kuwa makubaliano yamefikiwa.
Anaiita “sura mpya katika historia yetu”.
Muungano ni jambo ‘muhimu’ kwa DA – Steenhuisen
Steenhuisen anaelezea “kwa kiasi gani ni muhimu” kufikia makubaliano ya Muungano wa Kidemokrasia.
Ameongeza kuwa makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya “mazungumzo makali lakini yaliyokomaa mno” na kwamba yanaakisi sehemu nyingi za ilani ya DA.
Pia anasema makubaliano hayo ni “halisia katika haja ya mifumo ambayo bila shaka itatokea kwenye serikali ya vyama vingi”.
DA kumuunga mkono Ramaphosa kama raisi
Steenhusien amethibitisha kuwa chama chake kitamuunga mkono Cyril Ramaphosa kuwa rais ajaye wa Afrika Kusini.
Siasa mpya za ushirikiano – Steenhuisen
“Watu pia wametuambia kwamba wakati wa siasa mpya ya ushirikiano na utatuzi wa matatizo umefika,” Steenhusien amesema.
“Kuanzia leo DA itatawala kwa pamoja Jamhuri ya Afrika Kusini kwa moyo wa umoja na ushirikiano… tunafanya hivyo kwa ajili ya mamilioni waliopiga kura kwa ajili yetu na Waafrika Kusini wote wanaotamani serikali bora”, anasema.
Kilichoko mbele sio rahisi – Steenhuisen
Ingawa Steenhuisen amebainisha jinsi mpango huo ulivyo muhimu, pia anasema matatizo ya Afrika Kusini, kama vile uhalifu na masuala ya kiuchumi, “hayatatatuliwa mara moja” na kwamba “kilichoko mbele yetu sio rahisi.