Na Mwandishi wetu 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa wakazi wa maeneo yaliyoteuliwa kwa ajili ya majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo.

Zoezi hilo linalenga kupima utayari wa mifumo na vifaa vya uboreshaji wa daftari.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Tabora  tarehe 20 Novemba, 2023 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri amewapongeza wakazi wa mkoa huo kwa kupata fursa hiyo.

Alisema mkoa wa Tabora umekuwa ni miongoni mwa mikoa miwili ambayo kata zake zimeteuliwa kufanya majaribio hayo ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

Mhe. Mapuri amezitaja kata zitakazofanya majaribio hayo kuwa ni Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, ya mkoa wa Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, katika Mkoa wa Mara.

“Tume inawapongeza wakazi wa mkoa wa Tabora kwa mkoa wenu kuteuliwa kuwa mwenyeji wa zoezi,” alisema.

 

Mhe. Jaji Semistocles Kaijage aliteuliwa kuongoza Tume kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016 akichukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambaye muda wake wa kuwa Mwenyekiti umemalizika rasmi mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *