Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Afrika Kusini yamuondowa balozi na ujumbe wa wanadiplomasia wake Israel, ikiwa ni hatua ya kulaani mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Serikali ya Afrika Kusini imewaita nyumbani balozi wake na ujumbe wake wa kidiplomasia kutoka Israel, katika hatua ya kulaani mashambulizi yanayofanywa na nchi hiyo dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Afrika Kusini imeyaita mashambulio hayo kuwa mauaji ya halaiki. Serikali ya Afrika Kusini pia imetishia kuchukuwa hatua dhidi ya balozi wa Israel nchini mwake kufuatia matamshi  aliyoyatowa hivi karibuni  kuhusu msimamo wa nchi hiyo ya Afrika katika vita kati ya Israel na Hamas.

Hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa kuhusu matamshi ya balozi huyo wa Israel.

Waziri wa Afrika Kusini katika ofisi ya rais Khumbudzo Ntshavheni Afrika Kusini imeamuwa kuwaita nyumbani  wanadiplomasia wake wote kutoka Tel Aviv kwa ajili ya mashauriano.

Waziri wa mambo ya nje Naledi Pandor ambaye leo amemkaribisha mwenzake wa Ukraine   Dmytro Kuleba,amesema wanahitaji kushauriana na wanadiplomasia hao waliokuwa Tel Aviv kutokana na hali ya mauaji ya watoto inayowatia wasiwasi katika Ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *