Na Mwandishi Wetu, Kenya.
‘Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni’, hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwanaume kutoka mjini Maragua nchini Kenya kushikiliwa na Polisi baada ya kupeleka maiti ya mkewe akidai alimuokota shambani akiwa ameshafariki.
Naibu Kamishina wa Maragua, Joshua Okello, amesema mshukiwa alibeba maiti ya mkewe hadi kituo cha polisi na kudai alimwokota kutoka shamba la migomba.
Kwa mujibu wa majirani inadaiwa mwanaume huyo alimshambulia hadi kumuua mkewe usiku wa Agosti 19, 2023 kwa kosa la kuuza bangi ya kSh3, 000, (Sh51, 970)
