By Alice Komba, Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa jana Jumapili Julai 23, 2023 alisema kuna faida ambazo nchi itazipata kupitia Mafunzo ya Kimataifa ya Askari Wanawake wa Ukanda wa Afrika (IAWP).
Alisema kupitia mafunzo hayo yatawajengea uwezo askari wanawake na kuwaleta pamoja ambapo watabadilishana uwezo na uzoefu kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Afrika Kusini, Botswana, Ethiopia na Zimbabwe.
Akitaja faida zingine, Majaliwa alisema kuna fursa ya kujifunza utamaduni ili kuimarisha uhusiano ambao kimsingi askari watapata maarifa katika utendaji wao wa kila siku.
Majaliwa aliyasema hayo jana kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Kimataifa ya Askari Wanawake ukanda wa Afrika (IAWP), yaliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Majaliwa ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliwashukuru nchi washirika kwa kuichagua Tanzania kufanyia mafunzo hayo ya nne tangu kuanzishwa.
Uzindunzi huo wenye azma ya kuwajengea uwezo askari hao wanawake ulihudhuriwa na wageni zaidi ya 2,000 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Aidha alipongeza mafunzo hayo kupitia kauli mbiu ya mwaka huu wa 2023 isemayo, ‘Huduma kwa jamii kupitia uwezeshaji wanawake katika utekelesaji wa sheria’
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa