Na Mwandishi Wetu
Meneja Mkuu wa hoteli ya Blue Sapphire iliyoko Vingunguti Ilala jijini Dar es Salaam, ambaye ni raia wa kigeni, Salmat Laza anafanya unyanyasaji wa wafanyakazi wa hoteli hiyo.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar POST, anatumia lugha mbaya kwa wafanyakazi kwa misingi ya rangi, jinsia na utaifa.
Wakizungumza na Morningstar POST, kwa masharti ya kutokutajwa majina yao, wafanyakazi wa hoteli hiyo walisema kuwa meneja huyo raia wa India mwenye asili ya Pakstani, amekuwa akitumia nafasi yake ya kazi kuwafukuza kazi wafanyakazi bila kufuata taratibu za ajira.
Walisema kuwa mfanyakazi mmoja aliyefahamika kwa jina la Isack, alifukuzwa kazi na meneja huyo kwa tuhuma za kuiba kuku wakati tukio hilo la wizi lilitokea akiwa hayupo kazini na hakupewa nafasi ya kusikilizwa aliporipoti kazini.
Walisema kuwa Isack alifukuzwa kazi wakati aliyekutwa na kuku aliyeibwa ni Abushiri ambaye hakufukuzwa kazi na baadae alihamishiwa kitengo cha jikoni kwenye hoteli hiyo.
Waliongeza kuwa meneja huyo anafanya upendeleo kwa wafanyakazi wenye asili ya kihindi na kuwabagua wafanyakazi wengine kwa misingi ya utaifa na rangi.
Wafanyakazi wamekuwa wakilazimisha kufanya kazi mfulilizo wakiwa wamesimama bila kupumzika hata pale ambapo kuna kuwa hakuna wateja wa kuwahudumia.
Wafanyakazi wa hoteli hiyo wameeleza kuwa meneja huyo anawanyanyasa anawavunja moyo wa kufanya kazi kwa lugha mbaya na dharau kwa sababu mfanyakazi akitokea akaugua na kutokufika kazini hata pale anaporipti kazini akiwa na cheti cha daktari (sick sheet), anakatwa malipo yake ya mshahara kinyume na taaratibu za ajira.
Walieleza wasiwasi wao kuwa baadhi ya taratibu zingine zinakiukwa na meneja huyo kwa kuwa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la SUNSTAR LIMITED badala ya kutumia namba aliyosajili kwa jina lake au ya hoteli ya Blue Sapphire.
Habari za uchunguzi zinasema kuwa kampuni ya SUNSTAR LIMITED ambayo meneja huyo amesajili namba ya simu kwa jina hilo, inatumika tu kupokea malipo ya wateja wanaopata huduma kwenye hoteli hiyo.
“Hatuna uhakika kama kuna uhalali wa kufanya hivyo ni bora mamlaka husika zikachunguza jambo hili, je meneja huyo ameajiriwa na SUNSTAR LIMITED au hotel ya Blue Sapphire, kwa nini anatumia kampuni hiyo” walihoji wafanyakazi hao.
Pia, waliongenza kuwa kunawafanyakazi raia wa kigeni kwa jina la Gudu Gupta na Shubash, wanawasiwasi vibali vyao vya kufanya kazi vimekwisha hivyo wanaiomba mamlaka husika kufika hotelini hapo kufanya uchunguzi zaidi.
Akijibu tuhuma hizo Bw. Laza ambaye anadaiwa kufanya unyanyasaji sehemu za kazi, alikanusha kwa madai hayo na kusema kuwa yeye ni binadam hawezi kutumia lughu mbaya kwa watu.
“Je una rekodi yoyote inayoonesha kuwa nitumia lugha mbaya au kufanya unyanyaji” aliuliza Bw Laza na kuongeza kuwa mimi ni meneja nimefanya kazi muda mrefu na nina uzoefu wa kutosha nimeshafanya kazi kwenye hoteli nchini India inavyumba zaidi ya 200, alisema.
Alisema kuwa kuna wakati anapaza sauti baada ya kumuonya mfanyakazi zaidi ya mara mbili mfululizo, lakini anajitahidi sana kufanya kazi na wafanyakazi wote bila manyanyaso.
Bw. Laza alisema kuwa wafanyakazi waliofukuzwa kazi mikataba yao imekwisha, lakini Isack alifukuzwa kwa madai ya kuiba kuku na mfanyakazi mwingine Ratifa alimaliza mkataba wake na hakuwa tayari kuendelea na kazi.
Alisema kuwa hoteli hiyo inawafanyakazi zaidi ya 67 na wanafanya kazi hakuna unyanyasaji wowote na taaratibu zinafuata labda Isack anaweza kumrudisha kama kuna makosa yalijitokeza.
Akijubu madai ya wafanyakazi wenye asili ya India wanaofanya kazi vibali vikiwa vimekwisha alisema kuwa habari hizo si za kweli”(that is wrong information)” alisema Bw Laza.
Hata hivyo Morningstar POST inaendelea kumtafuta mkurugenzi wa hoteli hiyo anayedaiwa alikuwa nje ya nchi kwa mahojiano zaidi, na idara zingine za serikali kuzungumzia taarifa hizo.
.
Hoteli ya Blue Sapphire iliyoko Vingungu jijini Dar