Na Mwandishi Wetu

Jengo la ghorofa tatu la shule ya Awali na Msingi ya Willgrace iliyoko maeneo ya Kipawa Mpya Kata ya Pugu Ilala jijini Dar es Salaam, linajengwa bila kuhusisha mkandarasi wa ujenzi, Morningstar POST imebaini.

Jengo hilo linalodaiwa kuwa ni bweni kwa ajili ya watoto wa shule limejengwa mpaka kufikia ghorofa tatu bila kuwepo na bango kwenye eneo la mradi linaloonesha wakandarasi wanaohusika na ujenzi wa mradi huo.

Mradi huo umejengwa bila kusajiliwa kwenye Bodi ya Wakandarasi Nchini (CRB), na Bodi ya Wahandishi (ERB), ambazo zinaonesha kulala kwani majengo mengi yanajengwa jijini Dar es Salaam bila kusajiliwa na bodi hizo.

Licha ya kuhatarisha usalama wa watumiaji wa majengo hayo pia bodi hizo zinaikosesha serikali mapato ambayo yangetokana na usajili wa miradi ya ujenzi.

Akizungumza kwa niaba ya meneja wa shule hiyo Grace George, bwana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Sangijo, alisema kuwa hawana haja ya kutafuta makampuni ya wakandarasi kwa kuwa ni mradi wa ujenzi wa shule binafsi na sio za serikali.

“Hatuoni haja ya kutangaza tenda za kutafuta wakandarasi tunafanya wenyewe tu kwa kushirikiana na mainjini walioko serikalini….kwa kuwa na sisi wenye tuko kwenye mambo hayo hayo (serikali)” alisema.

Akaongeza “Vibali vya ujenzi tunavyo na sisi tuko kwenye mambo hayo hayo ya serikali” alijitapa Bw Sangijo.

Meneja wa shule hiyo Bi Grace, akizungumza na Morningstar Post kwa njia ya simu, hakutaka kuzungumza zaidi na kusisitiza kuwa Bw Sangijo ndio msemaji wao.

Juhudi za kuwapata viongozi wa CRB na ERB kuzungumzia mradi huu pamoja na viongozi wa serikali hazikuweza kufanikiwa mara moja hata hivyo tutaendelea kuwatafuta.

0713685823

Mradi wa shule ya awali na msingi unaojengwa maeneo ya Kipawa Mpya Kata ya Pungu bila kuwa na mkandarasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *