Na Mwandishi Wetu
Wafanyakazi wa kampuni ya Ujenzi ya Serikali ya China, China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), wamelalamikia uongozi wa kampuni hiyo kutokutenda haki kwa kuficha mikataba ya wafanyakazi wake.
Wakizungumza na Morningstar POST kwa mashariti ya kutokutajwa majina yao, walisema kuwa uongozi wa kampuni hiyo inayojenga mradi mkubwa wa ujenzi wa kituo cha biashara Ubungo jijini Dar es Salaam, East Africa Commercial and Logistics Centre (EACLE) hawatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wakaiona wanaambiwa kusaini fomu bila kuoneshwa mikataba yao.
Walisema kuwa licha ya kuwa mikataba ni makubaliano ya pande mbili kati ya mfanyakazi na mwajiri, lakini kampuni hiyo wanasema tu kuwa mikataba ipo lakini mfanyakazi honeshwi mkataba yao wanapewa tu fomu wanajaza bila kupewa mkataba wakasoma vipengele vilivyoko kwenye mkataba.
Pia alisema kuwa wafanyakazi wanafanyishwa kazi masaa mengi zaidi ya masaa ya kazi bila kulipwa malipo ya ziada.
Wakaongeza kuwa wafanyakazi wa kitanzania wanabaguliwa kwa kukatazwa kuvuta sigara wakati wachina wanaruhusiwa kuvuta sigara na iwapo mtanzania akivuta sigara anafukuzwa kazi.
Aidha wamelalamika zaidi kuwa baadhi ya wafanyakazi wanakatwa michango ya NSSF wakati hawana namba za NSSF.
“Tunakatwa malipo ya NSSF wakati hatuna namba za NSSF tunashangaa fedha zinakatwa wapi…kuna mwenzetu alikuwa anavuta sigara akafukuzwa akiwa hana namba ya NSSF sasa malipo yake atapataje” alihoji mmoja wa wafanyakazi hao.
Akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo, afisa mmoja wa kampuni kutoka ofisi ya Rasilimali Watu ambaye hakutaka kujitabulisha, alisema kuwa makato ya NSSF yanakatwa kwa wafanyakazi wote pamoja na wale wasiokuwa na namba wakishapata namba wanaingiziwa malipo yao.
Akizungumza na Morningstar Post Msimamizi wa Mkuu wa NSSF Ubungo ambaye hakutaka kujitambulisha kwa kuwa si msemaji wa NSSF, alisema kuwa mwajiri anawajibu wa kujiandikisha NSSF na kukata michango ya wafanyakazi wake kwa mujibu wa sheria.
“Mwajiri anawajibu wa kukata malipo ya wafanyakazi wake na kuwasilisha NSSF….tunayo akaunti maalum ambayo mwajiri anaweza kuweka michango ya wafanyakazi kisha mfanyakazi akishaandikishwa analeta taarifa zake tunamwekea malipo yake,” alisema.
Akito ufafanuzi zaidi anasema kuwa mfanyakazi anakatwa malipo kutokana na kipato cha mshahara na malipo ya ziada pamoja na malipo ya kuachishwa kazi anatakiwa kukatwa kwenye michango yake ya NSSF.
0713685823
Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki kinachoendelea kujengwa Ubungo jijini Dar es Salaam