Na Mwandishi Wetu

Wakazi wa Masaki jijini Dar es Salaam, wameeleza maskitiko yao kuhusu mtu mmoja anayefanya kazi serikalini kama Katibu Tawala wa Wilaya (DAS), kwa kutokuwa na mahusiano mazuri na wakazi wa maeneo hayo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao, walisema DAS huyo ambaye jina lake tunalihifadhi amekuwa akionesha dharau kubwa kwa majirani zake pamoja na uongozi wa serikali ya mtaa huo.

Waliongeza kuwa DAS huyo ambaye inadaiwa kuwa ameoa mtoto wa kigogo serikalini, amekuwa hazungumzi vizuri na wafanyabishara wa mtaani kwake pamoja na majirani wenzake na kunapokuwa na vikao vya pamoja kutatua changamoto za mtaani kwake huwa haudhulii vikao hivyo.

Pia, wanasema kuwa wakati mwingine amekuwa akisigana na wafanayabiashara mtaani kwake hasa wale wanaouza vinywaji kwenye ‘grocery’ na baa akihisi kwamba wanampigia kelele.

DAS huyo amekuwa akijigamba kwa uwezo wa fedha na nafasi yake ya kazi na kwa kuwa mkewe anamahusiano na  kigogo mzito wa serikali.

Kiongozi mmoja wa serikali ya mtaa huo alipoulizwa kuhusu DAS huyo, alionesha kutotaka kuzungumza lolote na kuomba kutotajwa jina lake kwa kuwa DAS huyo anaweza kumletea matatizo kwenye kazi yake.

Mkazi mmoja wa mtaa huo ambaye anamiliki nyumba na anapangisha wafanyabiashara kwenye nyumba yake, alikataa kata kata kuzungumzia kuhusu suala hilo na kukata simu.

Hata hivyo Morningstar Post ilimtafuta Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, kutaka muongozo wa maadili ya viongozi wa umma wenye kutokuwa na mahusiano mazuri katika jamii, hakuweza kupatikana mara moja kwa sababu alikuwa katika shughuli ya maandalizi ya mwenge.

Morningstar Post inaendelea kumfuatilia DAS huyo ambaye anafanya kazi katika wilaya moja iliyoko katika mkoa wa Dar es Salaam, na baada ya kupata tarifa kamili tunaendelea kuwahabarisha wasomaji wetu.

Wakazi wa Masaki wakiwa kwenye mkutano wa kujadili changamoto za mtaa wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *