0784663087

Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam (DMO), Elizabeth Nyema, amesema jiji la Dar es Salaam halina ugonjwa wa kipindupindu.

Bi. Nyema ametoa kauli hiyo kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa kipundupindu kimelipuka maeneo ya Kivule Ilala Dar es Salaam.

Amesema kuwa hakuna mgonjwa wa kipindupindu aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo waliofikishwa katika zahanati ya Kivule.

Alisema wagonjwa walifika kwenye zahanati hiyo ya Kivule walikuwa wanaharisha katika hali ya kawaida.

“Hakuna mgonjwa wa kipindupindu jijini Dar es Salaam hata mmoja
waliofikishwa hosptali walikuwa wanaumwa kawaida, kama kungekuwa na mgonjwa wa kipindupindu serikali ingetangaza kupitia kwa waziri wa afya,” alisema Bi Nyema.

Alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa zililenga kuleta taharuki kwa wananchi wa jiji la Dar e Salaam ili watu washindwe kufanya kazi zao kwa amani na uhuru.

Bi. Nyema amewataka wananchi kuendelea kufanya shughuli zao kama kawaida kwani katika jiji la Dar es Salaam hakuna mgonjwa hata mmoja wa kipindupindu.

Hata hivyo taarifa za kuibuka ugonjwa wa kipindupindu zimewashtua
baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao kwa muda mrefu hawajakumbana na ugonjwa huo.

Licha ya Mganga Mkuu wa Ilala kukanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu katika jiji la Dar es Salaam, taarifa hizo zichukuliwe kama chachu ya kudhibiti na kusimamia hali ya usafi katika jiji la Dar es Salaam ambalo baadhi ya maeneo hali ya usafi sio ya kuridhisha.

Katika jiji la Dar es Salaam kumekuwa na baadhi ya maeneo kuna marundikano ya uchafu   muda mrefu bila kuondolewa, maji machafu yamekuwa yakitiririka hovyo hususani katika maeneo ya katikati ya jiji.

Viongozi wa jiji wanapaswa kutambua kuwa kipindupindu ni matokeo ya uchafu, hivyo kudhibiti uchafu na kuelimisha umma kufuata kanuni za afya kutasaidia kuondoa tatizo la kulipuka kwa magonjwa kama kipindupindu mara kwa mara.

Hivi karibuni kumeibuka taarifa kuwa kipindupindu kimeibuka Dar es Salaam maeneo ya Kivule nje kidogo ya jiji watu zaidi ya 20 wamelipotiwa kufikishwa katika zahanati ya Kivule Ilal

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *