Watu wengi ukiwauliza swali biashara ni nini watakuletea maelezo yanayofundishwa kwenye vyuo na sehemu mbalimbali kuwa biashara ni kuuza na kununua huduma au bidhaa. Ni kweli hii ndiyo tafsiri na maana halisi ya biashara.

Katika biashara lazima kuwepo na muamala wa kuuza na kununua bidhaa au huduma kwa mabadilishano ya fedha au bidhaa.

Hata hivyo ukienda mbali zaidi na kuchunguza kwa kina maana ya biashara kama ambavyo wajasilimali wakubwa duniani kama vile Brayn Trace anasema biashara ni ile yenye kuleta utatuzi wa matatizo ya walengwa wako.

Kimsingi biashara ambayo haiwezi kutatua matatizo au changamoto za watu au walengwa wako hii ni biashara iliyokufa haiwezi kupiga hatua na kukua katika kwango kizuri.

Wateja au watu wanaonunua bidhaa au huduma hawanunui kwa sababu wanahitaji kununua kutoka kwako bali wananunua ili kutatua matatizo yao.

Biashara ziko za aina nyingi lakini katika makala haya ntaeleza aina moja ya biashara ambayo ni biashara ya kitaalam na jinsi unavyoweza kufanya biashara bila mtaji mkubwa.

Ninapozungumzia bila mtaji nina maana kila kitu unachotakiwa kufanya katika biashara ni mtaji, unapotenga muda wa kushughulikia biashara yako ni mtaji, unapotumia nguvu zako kutengeneza biashara yako ni mtaji.

Biashara ya kitaalam ni nini?

Watu wengi wakisikia neno mtaalam wanapata hisia za kuwa na vyeti vya diploma au degree. Ni kweli kuwa mtu aliyehitimu mafunzo na kutunukiwa vyeti anaweza kuwa mtaalam.

Lakini pia mtu anayefahamu jambo fulani kwa kina bila ya kuwa na cheti pia anaweza kuwa mtaalam. Mfano wavuvi wangapi wanavua samaki lakini hawana vyeti vya uvuvi hao ni wataalam wa kuvua samaki.

Si maanishi hakuna umuhimu wa kusoma na kuwa na vyeti vya taaluma fulani nachozungumzia hapa ni maana ya utaalam.

Kabla sijazama ‘deep’ kueleza biashara ya kitaalam nieleze kwa kifupi mtaalam ni nani.

Mtaalam ni mtu mwenye ujuzi wa juu au maarifa fulani ya jambo fulani mfano masoko, tiba, aina hiyo ya ujuzi au maarifa ya juu inatokana na kujifunza katika njia rasmi shuleni au vyuoni au njia isiyo rasmi ya kusoma vitabu kufanya kwa vitendo au uzoefu wa kazi.

Biashara ya kitaalam ni ipi?

Kuwa na biashara ya kitaalam ni namna ya kubadilisha elimu, ujuzi au maarifa uliyonayo kuwa fursa ya kujipatia kipato kwa kuanzisha huduma au bidhaa kuhusiana na utaalam wako.

Aina hii ya biashara ni ya kipekee na mbinu ya kutoa maarifa uliyonayo kwa kundi fulani la watu kupitia kutoa elimu ya kile ulicho na utaalam nacho.

Biashara ya kitaalam inaweza kujengwa katika ujuzi na maarifa mbalimbali kama jinsi ya kutengeneza tovuti, jinsi ya kupika, jinsi ya kutoa tiba fulani, jinsi ya kutengeza bidhaa nk.

Vile vile biashara ya kitaalam inaweza kuelezwa kwa namna tofauti mfumo tofauti mfano.Ushauri (consultation), Ualimu (Coaching) Uzungumzaji (Speaking), Mafunzo (Training).

Jinsi ya kuanzisha biashara bila mtaji unahitaji kufahamu aina hii ya biashara ya kitaalam kwani haihitaji mtaji mkubwa kama ambavyo unavyoweza kuuza bidhaa za kawaida.

Unachotakiwa kufanya kuweza kuanzisha biashara ya kitaalam ni kufanya utafiti wa soko na kubaini changamoto kubwa zinazowakabiili walengwa wako, baada ya hapo ni kujifunza na kupata suluhisho la matatizo yao na kuanza kuwauzia utatuzi wa matatizo yao.

Nirahisi sana kuanza kufanya biashara ya kitaalam bila kuwa na mtaji mkubwa.

Kama umefaidika na makala haya na ungependa kupata mwongozo wa jinsi ya kuanzisha biashara ya kitaalam bila kuwa na mtaji mkubwa tuma neno biashara kwenda whatsapp namba ifuatayo:

0744499499

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *