Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Balozi Mahmoud Kombo (Mb.) ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, uliofanyika kwa njia ya mtandao Desemba 9, 2024.

Mkutano huo umejikita kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) hususan bajeti ya misheni ya kanda iliyopo nchini humo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Desemba 2024 hadi Desemba 2025.

Aidha, taarifa ya kikao hicho itawasilishwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kitakachofanyika Desemba 11, 2024 na kuongozwa na Rais Samia Suluhu, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *