NA MWANDISHI WETU

Vyama vya upinzani nchini sasa vinazungumza namna ya kuunganisha kukabiliana na uenguaji wa wagombea wao walio wasimamisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hadi kufikia mchana wa siku ya Jumatatu, ACT Wazalendo walikuwa wamepata majibu ya asilimia 90 ya mapingamizi waliyokuwa wameweka dhidi ya kuenguliwa kwa wagombea wao.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, sehemu kubwa ya mapingamizi yao yametupiliwa mbali, isipokuwa asilimia kubwa katika majimbo ya Kigoma mjini na kiasi Tunduru ambapo wamefanikiwa kuwarejesha wagombea wao.

Kufuatia hali hiyo, Shaibu amesema kiongozi wa chama chao Dorothy Semu aliwasiliana na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuangalia namna ambayo vyama vya upinzani vilivyoathirika na uenguaji wa wagombea vitashirikiana kukabiliana na changamoto hiyo.

“Hili jambo kwa maoni yetu ni zaidi ya chama kimoja kimoja. Na kwa bahati nzuri kiongozi wetu wa chama ni Makamu Mwenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD) amekwisha wasiliana na mwenyekiti ambaye ni ndugu Freeman Mbowe kwamba ni wakati mwafaka sasa tukutane kwa dhalula na kwa maoni yetu si zaidi ya kesho. Na kwa bahati nzuri CCM ni sehemu ya kituo hiki.” Amesema Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo

TCD ni jukwaa lililoanzishwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni ili kushirikiana katika kujenga na kuimarisha utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi kupitia majadiliano, mashauriano, kupanga mikakati, na kutekeleza ajenda ya maendeleo ya kidemokrasia nchini

Shaibu amesema mapendekezo ya ACT Wazalendo katika muktadha wa kushirikiana chini ya jukwaa la TCD yamepokelewa vizuri. Hata hivyo hajui ni lini hasa vyama hivyo vitakutana ili kuanza rasmi mchakato wa kushirikiana

Baada ya hatua kushindwa katika mapingamizi, vyama vya siasa vina fursa ya kukata rufa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *