BBC
Mkuu wa masuala ya ulinzi wa Uingereza asema Urusi ina idadi kubwa ya waathirika wa vita vya Ukraine mwezi huu
Kulingana na mkuu wa masuala ya ulinzi wa Uingereza, Huu ndio mwezi ambao Urusi inaongoza kwa kuwa na majeruhi wengi tangu vita ndani ya Ukraine vianze.
Sir Tony Radakin amesema vikosi vya Urusi vinapoteza takribani watu na waliojeruhiwa1,500 kila siku ndani ya mwezi Oktoba pekee, na kufanya idadi ya watu walioathirika kufika 700,000 tangu vita vianze mwezi Februari 2022.
Urusi haiweki wazi idadi ya watu waliofariki vitani, lakini viongozi wa masuala ya ulinizi wa mataifa ya Magharibi wamesema kuwa idadi ya waliofariki mwezi Oktoba ndio kubwa zaidi hadi kufikia sasa.
Katika kipindi cha BBC cha jumapili cha Laura Kuensberg, Sir Tony amesema kuwa raia wa Urusi wanalipia gharama kubwa katika uvamizi wa Putin.
Lakini ameongeza kwa kusema Urusi inatumia zaidi ya 40% ya matumizi yake ya Umma kwenye masuala ya ulinzi ambayo anasema ni unyonyaji mkubwa kwenye nchi hiyo.
Wafuasi wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump wanasema kuwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky huenda akahitaji kuachia ardhi fulani ili kufikia upatikanaji wa amani. Hata hivyo, Sir Tony alisema kwa uthabiti kwamba washirika wa Magharibi wamejitolea kusaidia Ukraine kwa muda wowote vita hivyo vitakavyoendelea.
“Huo ndio ujumbe ambao Rais Putin anatakiwa kuelewa na uhakika kwa Rais Zelensky”, alisema kwenye kipindi hicho.
Mapema wiki hii, Putin alimpongeza Trump kwa kushinda uchaguzi mkuu na kusema madai ya Trump kuwa anaweza kumaliza vita ndani ya Ukraine yanahitaji kupewa kipaumbele zaidi.