Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Taifa, Mama Samia Suluhu Hassan

NA JONES MWAN’GONDA

Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho ni chama tawala ambacho kilinyakua viti vingi uchaguzi uliopita kufuatia kujitoa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Uchaguzi uliopita wagombea wa CCM walibaki wenyewe kwenye karatasi za kura na hatimaye kupata ushindi mnono, tofauti na mwaka huu ambapo wapinzani wanaweka wagombea wao wote wakiwemo Chadema ambao pia safari hii wanataka wanyakue ushindi wa viti kuanzia vitongoji ,vijiji na mitaa.

Nimetoa tahadhari kwa CCM kwa kuwa wametibuana sana kwenye uchaguzi wao wa kura za maoni, kuchagua wanachama walioomba kugombea kwa tiketi ya chama hicho.

Baada ya kumaliza chaguzi za kura za maoni kuliibuka malalamiko mengi kabla na baada ya matokeo. Wanachama wengi kwenye matawi mbalimbali nchi nzima. walilalamikia wasimamizi wa chaguzi hizo kwamba walipanga safu zao na kuwapitisha hata kama hawafai.

Malalamiko hayo yaliyotolewa na wagombea yalielezwa kwamba wanachama waliojiandikisha wengine hawakutoka maeneo yao kama kanuni za uchaguzi zinavyoelekeza kuwa wanachama lazima watokeo kwenye maeneo wanaoishi ndani ya matawi yao, lakini kuliibuka malalamiko wanachama wengine hawakutoka maeneo yao.

Malalamiko mengine ni waliopiga kura katika baadhi ya matawi wengine siyo wanachama wa CCM, walitafutiwa kadi za CCM kwa kuwapigia kura tu ndugu zao ili washinde na ilifikia mahali mpaka watu walipigana.

Sasa kwa yote hayo kama ngazi za juu za CCM zisipokuwa makini kusikiliza malalamiko hayo na kupatia ufumbuzi basi uwezekano wa kuwapitisha wanachama wasiofaa ni mkubwa matokeo yake wanaweza kushindwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

CCM toka utawala wa awamu ya tatu wa Hayati Benjamini Mkapa kilibadili kanuni za uchaguzi ndani ya chama chao kwa kuwakilishwa na wajumbe maalum waliokuwa wanachaguliwa kwa kufuata miongozo kuanzia kwenye mashina, matawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa.

Kwa wakati huo mpaka awamu ya tano CCM waliachana na kupiga kura za maoni kwa sifa za kuwa na kadi hai tu kwa kuwa waligundua kuwa mgombea mwenye uwezo kifedha anaweza kupandikiza wajumbe wengi na wasiojuana kwa kuwanunulia kadi ili wakampigie kura kwa nafasi atakayoitaka na hiyo ilipunguza malalamiko mengi.

Katika uongozi wa mama Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti CCM taifa, amerudisha kanuni za kila mwanachama hai mwenye kadi ya elekroniki au namba aliruhusu kupiga kura za maoni katika chaguzi za kutafuta wagombea watakaoiwakilisha CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kuanza hivi punde.

Sasa maswali wanayojiuliza wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM kama wala rushwa wakijipenyeza tena ndani ya CCM mstakabali wa chama chao utakuwaje?

Mpaka sasa mambo hayajawa mabaya sana japo malalamiko yako mengi ya wanachama hewa walioandaliwa kwa kupiga kura za maoni tu yaliyomlazimu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM taifa kutoa tamko kali kuwaambia wanachama wake kukubaliana na majina ya wagombea watakayoyarudisha kwa maslahi ya chama nakuwaunga mkono ili CCM ishinde kwa kishindo.

Aliwaomba wanachama kuungana na kusahau tofauti zao na kuvunja makambi rasmi ili wawe kitu kimoja. Je uchaguzi wa madiwani na wabunge utakuwa wa staili hii? tungoje majibu baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika.

+255 766 600 909

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *