NA MWANDISHI WETU

Baadhi ya watu wanafikiri chumba chenye muonekano wa hadhi ya hali ya juu, lazima utumie gharama kubwa kununua bidhaa za thamani kubwa.

Katika makala haya nta-share na wewe jinsi ya kufanya chumba cha kulala kuwa na muonekano wenye hadhi ya hali ya juu bila kutumia thamani na vifaa vya gharama kubwa.

Kutengeneza muonekano wa chumba cha hadhi ya hali ya juu bila kununua vitu vya thamani kubwa zingatia kufanya mambo yafuatayo:

*Matandiko ya kitanda na mito*
Chagua mtindo wa kupangilia mito ya kitanda kama inayotumika kwenye hoteli kubwa, chagua matandiko ya kitanda kama shuka, duveti, foronya, mito na chandarua viliovyotengenezwa kwa malighafi ya pamba ya hali ya juu yenye ufumwaji nyuzi kuanzia kiwango cha 200 hadi 300.

Jikitike zaidi kuchagua rangi za kawaida zisizokolea sana kama vile nyeupe au kijivu, huleta muonekano wenye hadhi, ‘lakshari’ na utulivu zaidi, piga pasi kila siku kuondoa mikunjo ya matandiko yako.

*Pangilia mito ya kitanda*
Tumia mito mikubwa ya mraba, weka nyuma ya mito ya kulalia kuongeza mwenekano kwenye kitanda, kisha ongeza mito midogo mbele ya mito mikubwa kuleta muonekano wa kuvutia zaidi, kitanda chako kisipungue mito sita mikubwa miwili na midogo.

*Funga taa za urembo*
Funga taa za urembo kwa juu ya dari ya chumba chako kwa kutumia kifaa maalum cha kunin’giniza taa ili kuleta muonekana mzuri wa chumba, zingatia chanzo cha taa zaidi ya moja na taa za pembeni ya kitanda ili kutengeneza muonekano wa rangi za mashuka kwa mwanga wa taa.

*Mpangilio na vifaa*
Ongeza kioo kikubwa cha kujitazama, kioo kizuri kilichowekwa sehemu nzuri ndani ya chumba, kinafanya mwanga wa taa kutengeneza muonekano wa kung’aa ndani ya chumba.

*Mpangilio wa rangi*
Jikite kwenye rangi mpauko, rangi zisizokolea sana hufanya chumba kuwa na muonekano wenye utulivu, zingatia sana rangi ya kijivu, blue, rangi ya dhahabu isiyokoza ili kuleta muonekano ghali wa chumba, epuka rangi zenye kukolea sana kama nyekundu inaleta hisia za kutisha na wasiwasi.

*Mpangilio wa thamani (Furnitures)*
Punguza makolokolo kwenye chumba cha kulala, weka mazingira safi ya chumba, pangilia vitu vizuri kuleta muonekano safi, epuka kuzidisha thamani kama makabati, viti, meza badala yake acha kila kimoja kijitegeme chenyewe.

*Funga pazia juu zaidi*
Kufunga mapazia juu zaidi ya dirisha karibu kidogo na dari kunaleta muonekano wa chumba kuonekana kirefu na kina nafasi na muonekana mzuri zaidi.

Kwa kuzingatia mambo haya unaweza kufanya chumba chako kuonekana chenye hadhi ya hali ya juu, na kuleta muonekano wenye utulivu unaochochea hisia za kupumzika zaidi kwenye chumba.

Kama utapenda kupata bidhaa kutoka HPM Collection kama mashuka, maduveti, mito, zuria usisite tuma ujumbe whatsapp ifuatayo
+255 754 243 110

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *