BBC
Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi, amesema Wademokrat wangeweza kufanya vyema katika uchaguzi wa Jumanne iwapo Rais Joe Biden angejiondoa katika kinyang’anyiro hicho mapema.
Pelosi – mmoja wa wanasiasa wenye nguvu huko Washington – aliliambia gazeti la New York Times kwamba “kama rais angetoka mapema, kungeweza kuwa na wagombea wengine katika kinyang’anyiro hicho”.
Matamshi yake ni lawama za hivi punde zaidi kutoka kwa Wanademocrat baada ya chama hicho kushindwa kuingia Ikulu ya White House na uwezekano wa mabunge yote mawili ya Congress mnamo Jumanne.
Pelosi anaripotiwa kuwa aliongoza msukumo wa chama cha Democrats kumtimua Biden, ambaye aliishia kuondoka kwenye kinyang’anyiro hicho mwishoni mwa Julai baada ya wiki za shinikizo kufuatia matokeo duni ya mdahalo dhidi ya Donald Trump.
Biden alipomaliza kampeni yake, alimuidhinisha haraka Makamu wa Rais Kamala Harris kuchukua nafasi yake. Alishindwa vibaya na Rais mteule Trump siku ya Jumanne.
Pelosi aliliambia gazeti la New York Times: “Matarajio yalikuwa kwamba, kama rais angejiondoa, kungekuwa na mchujo wazi.”
Uchaguzi wa mchujo wa wazi ungehusisha idadi ya wagombea wa Democtrat wanaoshindana kuchaguliwa na wajumbe wa chama kumrithi Biden.
Pelosi amesema kuwa Harris angefanya vyema katika mchakato wa msingi kama huu na ingemfanya “kuwa na nguvu zaidi mbele”.
“Lakini hatujui hilo. Hilo halikufanyika. Tunaishi na kile kilichotokea,”
“Na kwa sababu rais aliidhinisha Kamala Harris mara moja, hiyo ilifanya iwe vigumu kuwa na mchujo wakati huo. Kama ingekuwa mapema zaidi, ingekuwa tofauti.”