
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt Tulia Akson Mwansasu akisalimiana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin jijini St. Petersburg nchini Urusi.
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Mhe. Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo tarehe 12 Julai, 2024 viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.
Kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Dkt. Tulia amesema “Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi…”
Amesema: “Tumezungumza naye katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala”