Rais William Ruto

BBC

Hali inaonekana si shwari nchini Kenya maandamano dhidi ya serikali nchini Kenya yamegeuka kuwa ya vurugu huku wahalifu wakiteka nyara maandamano hayo.

Waandishi wa BBC wameshuhudia uporaji na uharibifu wa mali katika viunga vya Nairobi na katikati mwa jiji.

Mwanaharakati Boniface Mwangi na wengine kadhaa wamewataka vijana (GenZ,) kurudi nyumbani.

Mjini Mombasa, watu wawili wanadaiwa kuuawa na mwanaume anayedaiwa kuwa mfanyabiashara akitetea mali yake dhidi ya waporaji.

Rais Ruto alitupilia mbali mipango mipya ya ushuru, lakini maandamano yanaendelea kupinga ukatili wa polisi na uongozi wake.

Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha jijini Nairobi, huku maandamano madogo yakiendelea Mombasa na Kisumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *