KIMEUNGANISHA MFUMO WA MAJI TAKA KWENYE MFUMO WA MAJI YA MVUA*
NA MWANDISHI WETU
Kiwanda cha Cello kilichopo barabara ya Mbozi Temeke jijini Dar es Salaam, kinadaiwa kufanya uchafuzi mkubwa wa mazingira, Morningstar Post limebaini.
Kiwanda cha Cello kinadaiwa kuunganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji ya mvua kinyume na sheria za jiji.
Chanzo cha habari cha kuaminika kimesema kuwa kiwanda hicho limeunganisha mfumo wa maji taka kutoka kwenye kiwanda hicho kuelekea kwenye chemba ya maji ya mvua (stom water).
Habari zinaeleza kuwa katika kiwanda hichoĀ mfumo wa maji taka kwenye mtaa barabara yaĀ Mbozi umeunganishwa kutoka kiwandani ambako mfumo wa maji taka hakuna katika eneo hilo kuna mfumo wa maji ya mvua.
Wenye majengo yote wanatakiwa kunyonya maji taka kupeleka kwenye mabwawa ya kuchakata maji (treatment ponds) ya Dawasa, lakini kiwanda hicho umeunganisha kinyume na sheria.
Baadhi ya watu waoliko kwenye maeneo hayoĀ wamelalamika hali ya uchafuzi wa mazingira inasababisha mlipuko wa magonjwa ikiwemo kipindupindu kwa kuwa maji taka yamekuwa wakifumuka mara kwa mara kwenye barabara hizo.
Mkurugenzi wa Cello Industries Ketan Khakhar, alipotafutwa kuzungumzia taarifa hizi hakutaka jibu lolote alisema yuko Mwanza na kukata simu alipotafutwa tena hakupatikana hadiĀ tunarusha taarifa hii.
Morningstar Post inaendelea kumtafuta kuzungumzia suala hili.