NA MWANDISHI WETU
Jengo la ghorofa lililoko mtaa Chang’ombe maeneo ya VETA linalomilikiwa na Supermarket ya Mr Discount limeunganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji ya mvua, Morningstar Post imebaini.
Chanzo cha habari cha kuaminika kimesema kuwa jengo hilo limeunganisha mfumo wa maji taka kutoka kwenye jengo hilo kuelekea kwenye chemba ya maji ya mvua (stom water).
Habari zinaeleza kuwa katika jengo hilo limeunganisha kwenye mfumo wa maji taka kwenye mtaa barabara ya Mbozi ambako mfumo wa maji taka hakuna katika eneo hilo kuna mfumo wa maji ya mvua.
Wenye majengo yote wanatakiwa kunyonya maji taka kupeleka kwenye mabwawa ya kuchakata maji (treatment ponds) ya Dawasa, lakini jengo hilo limekuwa likienda kinyumbe na sheria.
Baadhi ya watu waoliko kwenye maeneo hayo barabara ya Chuma wamelalamika hali ya uchafuzi wa mazingira inasababisha mlipuko wa magonjwa ikiwemo kipindupindu kwa kuwa maji taka yamekuwa wakifumuka mara kwa mara kwenye barabara hizo.
Mkurugenzi wa Mr Discount Khalid Maksoor, alipotafutwa kuzungumzia taarifa hizi hakutaka kupokea simu mara kadha, na kutaka kutumiwa meseji lakini hakujibu ujumbe wowote mpaka tunarusha taarifa hii.