NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deogratius Ndejembi
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deogratius Ndejembi amesema vikundi 102 vya Wanawake vyenye wanufaika 875 vinavyojishughulisha na kazi za ufugaji vimekopeshwa kiasi cha Shilingi Milioni 575.
Ndejembi ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Zodo aliyehoji Serikali ina mpango gani wa kuvisaidia vikundi vya uzalishaji mali vikiwemo vya ufugaji ambavyo wanawake wamehamasika ili waweze kufanya ufugaji wenye tija.
Alisema, Halmashauri za Mkoa wa Tanga na maeneo mengine nchini zimekua zikitoa mikopo ya uwezeshaji kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani. Mikopo hiyo imekua ikitumika kwenye shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo ufugaji.
“Kwa mwaka wa fedha 2021/22 na 2022/23, Halmashauri yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.5 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 1.8 zilikopeshwa kwenye vikundi vya Wanawake,” alisema Ndejembi.