Na Mwandishi wetu
Licha ya Serikali kuwahakikishia watanzania kuwa chanjo ya Covid-19, inayotolewa na serikali kwa ajili ya kujikinga na virus vya Covid-19 kuwa ni salama baadhi ya watu wamekuwa wakikwepa kuchanja chanjo hiyo.
Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA), ilitoa walaka kwa umma kuweka wazi na kuwatoa hofu wananchi kujitokeza kuchanja chanjo hiyo ambayo inatolewa hapa nchini kupitia zahanati mbalimbali za serikali na hospitali binafsi.
Katika taarifa ya TMDA, serikali ya Tanzania imekuwa kinara wa kutoa chanjo na imefanikiwa kudhibiti magonjwa yanayodhibitiwa na chanjo kama vile ugonjwa wa ndui, pepopunda kwa watoto wachanga na ugonjwa wa kupooza (polio).
Licha ya serikali kusema kuwa imekuwa ikihakikisha usalama wa chanjo zote zinazoingizwa nchini ni salama, ufanisi na ubora pia chombo udhibiti wa dawa TMDA inatambuliwa Shirika la Afya Duniani kwa udhibiti wa dawa na chanjo.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ugonjwa wa COVID-19 umeathiri watu 188,310, 329 na kusababisha vivyo 4,053, 803 duniani kote.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa mwandishi wa makala haya ambaye ametembelea na kuhoji baadhi ya watu na kufanya uchunguzi kwa kuchukua huduma katika baadhi ya zahanati za serikali na hospitali binafsi amebaini kuwa chanjo za COVID-19 zinatolewa bila watu kuchanja na kupatiwa vyeti.
Kutokana na baadhi ya nchi duniani kuweka masharti ya kuingia katika nchi hizo bila kuwa na uthibitisho wa vya vyeti vya chanjo ya COVID-19 imepelekea baadhi wa watu wasiotaka kuchanja chanjo hiyo kufanya udanganyifu kwa kushirikiana na watendaji wa vituo vya afya kupewa vyeti vya Covid 19 bila kuchanja.
Morningstar Post inaendelea kufuatilia baadhi ya hospitali binafsi zinajihusisha na kutoa vyeti vya chanjo ya COVID-19 bila watu kuchanja na kuchapisha orodha ya hospitali hizo.