Nyumba iliyoko Kibena Kata ya Vijibweni iliyoko kwenye mgogoro na inadaiwa kuwa inatakiwa kuporwa na watu wanadai kuwa ni wamiliki wa eneo hilo.

Na Mwandishi Wetu

Mkazi wa Kibene Kata ya Vijibweni, Wilaya ya Kigamboni, Fedel Nzakaha bado anaendelea kutetea haki yake baada ya kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga maamuzi ya kuporwa nyumba yake (pichani).

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao hawakupeda kutaja majina yao, wamesema wanafahamu kuwa nyumba hiyo iko kwenye mgogoro kwa muda mrefu.

Walisema kuwa nyumba hiyo wanafahamu kuwa ni mali ya Bw Nzakaha amekuwa jirani yao kwa muda mrefu sana tangu anaanza kujenga nyumba yake wamekuwa wakimuona hapo.

Wakizungumzia mgogoro unaofukuta katika nyumba yake walisema kuwa suala hilo lilianza mwaka 2018, waliibuka watu wakidai kuwa eneo hilo ambalo Bw Nzakaha amejenga kuwa ni eneo lao.

Walisema kuwa mgogoro huo ulizungumzwa kwenye ofisi za serikali ya mtaa na hatimaye kuibukia kwenye Baraza la Ardhi la Wilaya Temeke ambako lilisikilizwa na kufikishwa Mahakama Kuu.

Akizungumza na Morningstar Post, Bw. Nzakaha, alisema kuwa watu waliomuuzia eneo hilo wanajaribu kutaka kumpora nyumba yake kwa kuwa hawana vielelezo vinavyoonesha kuwa ni wamiliki halali wa eneo hilo lakini wamekuwa wakimsubua kwa miaka mingi.

Alisema kuwa yeye aliuziwa eneo hilo na Sylvester Ntayabarwa mwaka 2018, lakini baadaye watu hao waliibuka na kudai kuwa eneo hilo wanalihitaji wampatie sh15,000,000 awape eneo.

Anasema baada ya kukataa kutoa eneo hilo walimfungulia shauri Baraza la Ardhi, ambako pamoja na kuwasilishwa vielelezo vyote watu hao walipewa ushindi na  kuamua kukata rufaa mahakama kuu ambako shauri hilo bado linaendelea.

Hata hivyo, Bw Nzakaha alionesha kushangazwa na jinsi maamuzi ya baraza yalivyotolewa kwa kuwa siku ya hukumu shauri lilisomwa wakapewa ushindi baadae mweshimiwa peke yake bila kuwepo wazee wa baraza aliwapa ushindi walalamikaji.

Anasema kuwa shahidi aliyekuwepo wakati ananunua eneo hilo Bahati Maganga anaonekana kuwepo pia upande wa nyaraka zilizowasilishwa na watu hao wanaodai kuwa ndio wamiliki wa eneo hilo.

Hata hivyo Bw. Nzakaha  ameshakata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa kupinga maamuzi hayo yaliyotolewa na Baraza la Ardhi na Mhakama Kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *