Mbole ya pembejeo za kilimo.
Na Mwandishi Wetu
Pembejeo za kilimo zinazotolewa na Wizara ya Kilimo, kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo hapa nchini, zinauzwa nje ya nchi badala ya kukopeshwa wakulima wa ndani, Morningstar Post imebaini.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kinadai kuwa taasisi ambazo zimekuwa zikichukua dhamana ya kukopesha wakulima pembejeo za kilimo zimekuwa zikienda kinyume kwa kuuza pembejeo nje ya nchi badala ya kukopesha wakulima.
Habari zaidi zinasema kuwa taasisi hizo zimekuwa zikuuza nje ya nchi badala ya kuwakopesha wakulima kutafuta maslahi zaidi kwa manufaa yao binafsi.
Uchunguzi umebaini kuwa tayari wawakilishi kadhaa wa taasisi hzo zinazopewa dhamana ya kukopesha wakulima pembejeo za kilimo hapa nchini, zimekamatwa na jeshi la polisi na kuhojiwa.
Morningstara Post inaendelea na uchunguzi zaidi baada ya kuwasiliana na jeshi la polisi na baadhi ya taasisi na watu binafsi zilizohusika kufanya hujuma hizo tutaendelea katika chapisho lijalo
*Uratibu wa pembejeo za kilimo*
Mfuko wa Pembejeo ni taasisi ya Serikali inayotoa mikopo ya Pembejeo za Kilimo/Mifugo na Zana za Kilimo. Mikopo inayotolewa na Mfuko wa Pembejeo ni kwa ajili ya kupanua maeneo ya kilimo na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi.
Muda wa mikopo ni kati ya miaka miwili (2) hadi mitano(5) kutegemea aina ya mkopo. Riba ya mkopo ni asilimia sita (6%) hadi nane (8%) kutegemea aina ya mkopo.
Dhamana za mikopo ni hatimiliki au leseni ya makazi ya mali isiyohamishika kwa waombaji binafsi kampuni. Kwa Vyama vya Ushirika na Taasisi za Kijamii zisizo na dhamana zenye hati miliki au leseni za makazi za mali zisizohamishika, dhamana ni akiba za wanachama (30%) na Halmashauri husika (70%).
Fomu za maombi ya mikopo zinapatikana kwenye tovuti wizara ya wizara ya kilimo Ofisi za Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji. Mkopo utaanza kurejeshwa baada ya mwezi mmoja hadi sita. Fedha ya Mkopo italipwa kwenye Kampuni ya chaguo la mwombaji.