Na Emmanuel Lyimo

Madawa mbalimbali yanayosadikiwa kuwa hatari kwa binadam, yamehifadhiwa ndani ya hoteli ya Continental maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam, Morningstar POST imebaini.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar POST,  umebainika kiasi kikubwa cha madawa ya aina mbalimbali yemahifadhiwa kwenye hoteli hiyo iliyoko mtaa wa Nkrumah.

Habari za  kuaminika kutoka ndani ya hoteli hiyo, zinaeleza kuwa madawa hayo ambayo mengine yamekwisha muda wake na mengine bado hayajakwisha muda wake, yamehifadhiwa katika vyumba vilivyoko ndani ya hoteli hiyo.

Chanzo cha habari cha kuaminika kimeeleza kuwa madawa hayo yamekuwa yakifunguliwa na kutupwa kwenye vyoo vya hoteli hiyo .

Inaelezwa kuwa madawa yaliokuwa kwenye maboksi yamekuwa yakitupwa kwenye magari yanayopita hotelini hapo kuzoa taka na kupelekwa dampo.

Inadaiwa dawa hizo zimehifadhiwa hotelini hapo na raia mmoja wa China anayeendesha mgahawa wa vyakula vyenye asili ya China ambaye alifahamika kwa jina la Jane.

Mtoa habari hizi anadai kuwa wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi ya kufungua dawa hizo na kutupa vyooni waliathirika na madawa kwa kupata madhara  ya kukohoa.

Aidha, waandishi wa habari hizi walifika katika hoteli hiyo na kupiga picha dawa hizo hatua ambayo meneja wa hoteli hiyo aliyefahamika kwa jina la Ashura aliingilia kati na kuzui zoezi hilo.

Uchunguzi wa Morningstar POST imebaini kuwa hoteli hiyo inayomilikiwa na Mh. Betty Machangu.

Uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana madawa

Mgahawa wa Kichina ulioko mbele ya hoteli ya Continental inayodaiwa kuhifadhi madawa hatari

Madumu matupu ya dawa zilizomwagwa vyooni ambazo zilikuwa zimehifahiwa hotelini 

Maboksi ya madawa yanayodaiwa kutupwa dampo ambayo yalikuwa yamehifadhiwa hoteli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *