Na Emmanuel Lymo.
Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zimeendelea kusababisha kero kwa wakazi wa jiji hilo ikiwemo maeneo ya Mbagala Rangi Tatu.
Morngingstar Post imeshuhudia Ijumaa wiki hii kufurika kwa maji ya mvua maeneo ya barabara ya Kilwa kuanzia Zhakiem hadi Mbagala rangi tatu maji yamefurika na magari kupita kwa shida.
Hali ya barabara hiyo imeonekana kutoruhusu maji ipasavyo kwenda kwenye mifereji kutokana na kujengwa hovyo kwa vituo vya mabasi ambavyo pia maji yamekuwa yakituama kwenye barabara hizo.
Baadhi ya watu walikuwa wakikimbilia kujihifadhi kwenye vituo vya mwendokasi ambavyo navyo vilionekana kuvuja kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha.
Wakizungumza na Morningstar POST baadhi ya watu walisema kuwa maeneo hayo mvua hata kama sio nyingi maji yamekuwa yakijaa.
Wakaongeza kuwa ni hatari sana kupita na watoto wadogo wakati mvua ikiwa inanyesha.
“Kwa kweli tunaomba viongozi wanaohusika waangalie upya miundo mbinu ya maji hapa Mbagala wakati mafundi wanaojenga barabara waweze kurekebisha miundombinu hiyo”, alisema mkazi mmoja wa Mbagala aliyejitambulisha kwa jina la Micheal Kiluwa.
0712219883

Sehemu ya barabara ya Mbagala Zhakiem iliyofurika maji ya mvua