Kumekuwa na idadi kubwa ya watu wenye tatizo la nguvu za kiume haswa vijana na hali imekuwa ikiongezeka kila kukicha kutokana na mtindo mbovu wa maisha usiozingatia kanuni za afya.
Kutokana na hali hiyo, idadi kubwa ya watu wamekuwa wakijitokeza kuuza dawa za nguzu ya kiume hapa nchini na watu wamekuwa wakitumia dawa hizo bila kuelewa maana ya nguvu za kiume.
Baadhi ya madawa ya kuongeza nguvu za kiume yamekuwa yakitumiwa na vijana wengi hasa madawa kutoka Kongo ambayo yamekuwa yanasambaa sana na kuuzwa nchini.
Watu wengi wamekuwa wakitumia madawa hayo bila kujua athari za matumizi ya madawa ya nguvu za kiume ambayo yanatumiwa na vijana.
Kabla ya kueleza jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa kutumia vyakula na mazoezi ntaeleza kwa kifupi maana ya nguvu za kiume.
Nguvu za kiume ni hali ya mwanaume kuweza kushiriki kikamilifu tendo la ndoa bila kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo katika kutekeleza tendo la ndoa.
Iwapo mwanaume utakuwa na changamoto ya kuwahi kufika kileleni inaweza kuelezwa kuwa ni changamoto ya nguvu za kiume ambayo imekuwa ni tatizo kwa wanaume wengi.
Baadhi ya wanaume wamekuwa wakishindwa kurudia tendo la ndoa kwa muda mfupi na uume kusimama kwa ulegevu, zote hizo ni baadhi ya changamoto za nguvu za kiume.
Pia, hali ya mawanaume kushindwa kurudia tendo na kuchoka sana baada ya kushiriki tendo kwa mara ya kwanza inaweza kuwa ni upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.
Ziko changamoto nyingi zinazo wakabili wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume ambao wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku kulingana na mtindo mbovu wa maisha ambao wamekuwa wakiishi.
Hata hivyo, changamoto ya nguvu za kiume si uogonjwa kama ambavyo imekuwa ikifikiriwa, mwanaume mwenye changamoto za nguvu za kiume ni dalili ya kuwa afya yake ya mwili haiko sawa.
Iwapo mwanaume ana ugonjwa wa kisukari anaweza kukumbana na changamoto ya nguvu za kiume, iwapo mwanaume anauzito uliopitiliza anaweza kukabiliana na tatizo la nguvu za kiume.
Iwapo mwanaume ana magonjwa ya zinaa, UTI na matatizo ya kisaikolojia anaweza pia kukumbana na changamoto ya nguvu za kiume.
Pia, iwapo mwanaume misuli yake imedhoofika na kulegea pia anaweza kukabiliana na nguvu za kiume, kama mwanaume ameshiriki katika tabia ya kujichua kwa muda mrefu anaweza kukabiliana na changamoto ya nguvu za kiume.
Sababu zinazopelekea changamoto ya nguvu za kiume ni nyingi, lakini upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume si ugonjwa ni hali inayotokana na kukosekana kwa afya bora kwa mwanaume kulingana ulaji na mtindo mbovu wa maisha.
Katika makala haya ntakuleza jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa kutumia vyakula na mazoezi bila kutumia madawa ya asili, madawa ya kuongeza nguvu kama viagra na kadhalika.
Hatua ya kwanza kabla ya kuanza kushughulikia tatizo la nguvu za kiume kwa mwanaume unatakiwa kuhakikisha unacheki afya yako kwa ujumla kwa kuhakikisha hauna ugonjwa wa aina yoyote.
Pili, unatakiwa kuacha kufanya mambo yafuatayo; kuacha kabisa kujichua (punyeto), punyeto ya aina yoyote ile kuna aina nyingi za kufanya punyeto lakini ntaeleza kwa kina katika makala ijayo.
Vile vile, unatakiwa kuacha kabisa kuangalia aina yoyote ya video au picha za ngono, pamoja na kuacha kula vyakula visivyokuwa vya kiafya kama vile vyakula vyenye sukari nyingi, nafaka zilizokobolewa, soda, pamoja na kubadili mtindo wa maisha.
Katika makala haya ntakueleza baadhi ya matunda ambayo ukizingatia kula na kufanya mazoezi ya viungo yenye kuimarisha misuli ya uzazi, utaweza kuboresha afya ya uzazi na kuondokana na tatizo la nguvu za kiume.
Lakini, hakikisha unabadili mtindo wa maisha kwa kufuata kanuni za afya kama kula kiafya, kufanya mazoezi maalumu ya viungo na misuli ili kuongeza nguvu za kiume.
Parachichi, virutubisho vilivyoko kwenye tunda la parachini ni zuri kuna kirutubisho cha wanga aina fibre na lina mafuta salama yasio na cholesterol kwa mwanaume mwenye changamoto ya nguvu za kiume parachini ni tunda linalotakiwa kuwepo katika mlo wake wa kila siku.
Ndizi za kuiva, madini ya potasium yalioko kwenye tunda hili la ndizi ni muhimu kwa afya ya moyo hawa katika kudhibiti presha, watu wachache sana wanapata madini haya katika mlo wao wa kila siku.
Watu wanaokula ndizi wanapunguza asilimia 27 ya magonjwa ya moyo ambayo ndio msingi mkubwa wa ufanisi katika tendo la ndoa.
Mzunguko mzuri wa damu katika mwili una mchango mkubwa katika kuleta ufanisi katika tendo la ndoa, hali ya uume kusimama kwa ulegevu ni ishara kuwa mzunguko wa damu hauko vizuri.
Tikiti maji, ni tunda linasaidia pia katika kudhibiti magonjwa ya moyo kwa kiasi kikubwa linapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kupunguza kiwango cha cholestrol mwilini.
Tafiti zinaonesha kuwa kirutubisho cha lycopene kinasaidia kupunguza cholestral na kupunguza presha.
Tikiti maji pia lina madini ya citrulline, amino acid ambayo yanaongeza kiwango cha madini ya nitric oxide mwilini. Nitric oxide inasaidi kuifanya mishipa ya damu kutanuka na kupitisha damu kwa urahisi.
Kwa mwanaume mwenye changamoto ya nguvu za kiume unapaswa kuhakikisha kuwa tikiti maji linakuwa miongoni mwa mlo katika mlo wako wa kila siku.
Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa tatizo la nguvu za kiume linaweza kuondoka kwa kuzingatia vyakula, mazoezi na kuacha mtindo mbovu wa maisha na sio kwa kutumia madawa ya kuongeza nguvu za kiume.
Kama umefaidika na makala haya comment nimefaidika na kama utapenda kupata muongozo wa vyakula na mazoezi muhimu kuboresha tatizo la nguvu za kiume tuma ujumbe nguvu kwenda namba
0744 499499
