Na Atley Kuni, WAF-DODOMA
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb.) amezindua gari maalumu la Kliniki tembezi ya Magonjwa ya Saratani kwa Wanawake kwenye Hospitali ya Kanda Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma huku shabaha ikiwa nikuwafukia wakimama mama waliowengi vijijini.
Akizindua gari hilo Mhe. Mchengerwa amewataķa Watumishi wa Afya kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidii, moyo wa kujitoa na maaarifa ili watanzania wapate huduma zenye tija.
“Jiepusheni na vitendo viovu vinavyoweza kuichafua BMH na Serikali kwa ujumla kama vitendo vya Rushwa, toeni huduma bora kwa mteja, lugha nzuri; Mkurugenzi Mtendaji endelea kuwakumbusha watumishi kila wakati juu ya Wajibu wao, vikao vya kukumbushana majukumu na wajibu wa watumishi wote vifanyike” amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Ametaka watamushi wa BMH kutambua kuwa wana wajibu wa kufanya kazi asubuhi, mchana na usiku ili matokeo yaonekane ambayo yatasaidia na kuwashawishi watoa maamuzi kwenye mchakato wa kuipa hadhi BMH kuwa Hospitali ya Taifa.
Akiongea katika hafla hiyo, Mratibu Mkazi wa mradi mtambuka wa Saratani za wanawake Afrika Mashariki Dkt. Sara Maongezi amesema kuwa, mradi huo ni wa miaka minne (4) kuanzia mwaka 2025 huku ukilenga kupunguza madhara yatokanayo na saratani kwa wanawake ikiwemo kuboresha vituo vya saratani na kugawa vifaa vya matibabu ya saratani ikiwemo kliniki hiyo tembezi yenye thamqni ya shilingi Milioni 272 za Kitanzania.
“Kliniki tembezi tunayoitoa ni kwa ajili ya kuwezesha uchunguzi wa saratani ya shingo ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti kwenye maeneo ya vijijini ambapo wakina mama hawawezi kufika Hospitali kwa urahisi kwa mjini, amesisitiza Dkt. Maongezi.
Awali akimkaribisha Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Prof. Abel Makubi amesema kuwa mradi huo ni muendelezo wa makubaliano ya ushirikiano (MOU) ambao tulisaini na Taasisi ya Afya ya Aga Khan mwaka 2025 kwenye maeneo ya mafunzo, utafiti na matibabu, ambapo mradi utasaidia kuhudumia wananchi takribani mil 14 wa mikoa ya Dodoma na inayozunguka Kanda ya Kati kwa ujumla.