WAZIRI wa Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amekagua eneo ambalo zitafanyika sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) mwaka huu na kuridhishwa na maandalizi.

Sherehe hizo zinatarajia kufanyika Manispaa ya Singida.

Akizungumza baada ya kuangalia maandalizi hayo, jana Aprili 22,2025, Waziri Kikwete alisema, yanakwenda vizuri na hatua iliyopo sasa ni zaidi ya Asilimia 88.

“Ninawashukuru sana Viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Katibu Mkuu Ndg. Henry Mkunda kwa kazi nzuri akishirikiana na uongozi wa Mkoa chini ya Cde. Halima Dendegu,” alisema na kuongeza kuwa, Mei Mosi hii inakwenda kupeleka Neema na mabadiliko makubwa Mkoa wa Singida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *