
MWANDISHI WETU
Wakati wakazi zaidi ya 200 Mtaa wa Yombo Dovya Uliopo Kata ya Makangarawe Temeke Jijini Dar es salaam kudhurika kwa Kutumia Mafuta ya Kupikia waliyonunua Dukani, sukari isiyofaa kwa matumizi ya binadam yauuzwa.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Morningstar Post, sukari hiyo iliagizwa nchini na kampuni kubwa maarufu ambayo tunahifadhi jina lake kwa sasa.
Uchunguzi umebaini kuwa sukari hiyo, baada ya kuingizwa nchini ilionekana kuwa haifai kwa matumizi ya binadam, hivyo kampuni iliyoagiza sukari hiyo ililipwa bima.
Hata hivyo kampuni ya bima ambayo ni kampuni mwenza wa kampuni iliyoagiza sukari hiyo ilianza kuuza sukari hiyo kwa wafanyabiashara mbalimbali.
Sukari hiyo imeenea katika maeneo ya Mbagala zaidi ambako wafanyabiashara wameuziwa.
Morningstar Post inaendelea kufanya uchunguzi zaidi baada ya kupata taarifa zaidi itaweka wazi wote waliohusika kuagiza na kuuza sukari hiyo.