MWANDISHI WETUMANYARA:

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimetakiwa kuwalinda wawekezaji hususani wa ndani ya nchi ili wasikwame katika suala la uwekezaji.

Pia kituo hicho kimetakiwa kuwawezesha wawekezaji pale panapostahili ili kukuza sekta ya uwekezaji nchini.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo.

Prof Mkumbo ametoa maagizo hayo hii leo Jumapili Januari 5, 2025 alipotembelea kiwanda cha Mati Super brands Ltd kilichopo mkoani Manyara kinachomilikiwa na mwekezaji mtanzania David Mulokozi.

Amewataka TIC kuwatazama wawekezaji kwa jicho la kipekee na kuhakikisha hawakwami kwa namna yoyote ile katika kufanikisha shughuli zao za kiuwekezaji.

“Niwaelekeze TIC wawekezaji kama hawa muwape jicho la pekee uwekezaji wao usikwame hata dakika moja,”amesema prof Mkumbo.

Aidha, katika hatua nyingine Prof Mkumbo amewataka TIC, kuwawezesha wawekezaji kwa namna yoyote ile ili kuhakikisha wanafanikisha uwekezaji wao na kuliingizia taifa kipato huku akihaidi serikali kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji nchini na kuahidi kuwasikiliza pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali.

“kile ambacho wanachotaka kufanikisha tuwawezeshe wafanikiwe na tuwahaidi sisi kama serikali kuendelea kuwekeza mazingira wezeshi kwa wawekezaji hapa nchini,”amesema prof Mkumbo.

Prof Mkumbo amehitimisha rasmi ziara yake hii leo Januari 5, 2025 mkoani Manyara ambapo ametembelea kiwanda cha uzalishaji bidhaa changamshi(vileo) cha Mati Super brands Ltd kinachomilikiwa na mwekezaji wa ndani David Mulokozi ambapo kitila ametumia nafasi hiyo kumpongeza kwa uwekezaji huo mkubwa na kuahidi serikali kushirikiana naye kwa ukaribu

Aidha, katika hatua nyingine Prof Mkumbo amewataka TIC, kuwawezesha wawekezaji kwa namna yoyote ile ili kuhakikisha wanafanikisha uwekezaji wao na kuliingizia taifa kipato huku akihaidi serikali kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji nchini na kuahidi kuwasikiliza pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali.

“Kile ambacho wanachotaka kufanikisha tuwawezeshe wafanikiwe na tuwahaidi sisi kama serikali kuendelea kuwekeza mazingira wezeshi kwa wawekezaji hapa nchini,”amesema prof Mkumbo.

Prof Mkumbo amehitimisha rasmi ziara yake hii leo Januari 5, 2025 mkoani Manyara ambapo ametembelea kiwanda cha uzalishaji bidhaa changamshi(vileo) cha Mati Super brands Ltd kinachomilikiwa na mwekezaji wa ndani David Mulokozi ambapo kitila ametumia nafasi hiyo kumpongeza kwa uwekezaji huo mkubwa na kuahidi serikali kushirikiana naye kwa ukaribu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *