Na Jones Mwang’onda

MAJENGO YA ghorofa yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa jijini dar es Salaam, baadhi yanajengwa bila kufuata taratibu na sheria za ujenzi.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari wabobevu wa tovuti ya habari ya Morningstar post umebaini.

Mwaka 2006 aliyekuwa Waziri Mkuu nchini, Hayati Edward Lowasa, aliunda tume ya kuchunguza majengo yote ya ghorofa jijini Dar es Salaam, ili kubaini majengo yasiyofaa au majengo yanayohitaji marekebisho kwa usalama wa watumiaji.

Kamati hii nakumbuka kwa wakati ule ilimpa sifa nyingi sana Mh.Lowasa ambaye pia alikuwa ni mbunge wa Monduli. Wakazi wa Dar es Salaam walitaka kupata matokeo ya majibuya tume iliyoundwa.

Ili waondokane na mashaka katika majengo waliokuwa wanayatilia mashaka, hata kwa muonekano wa majengo hayo.

Hii Leo Watanzania wamepata msiba baada ya kuporomoka kwa jengo lingine maeneo ya Kariakoo na kuleta majonzi makubwa sana kwa watanzania wote.

Nakumbuka kamati ile ya uchunguzi iliyoundwa na Lowassa, ilitoa majibu ya uchunguzi wake na ilibaini kuwa zaidi ya majengo 100 ya ghorofa yalijengwa chini ya kiwango na mengine mengi yalihitaji marekebisho/

Hata hivyo, kama ilivyo nchi yetu mambo yaliishia pale hakuna kilichofanyika na maghorofa mengi yanaendelea kutumika, je tutarajie nini juu ya kudharau maoni ya wataalam wa majengo?
Haikuishia hapo pia jiji la dar es Salaam liliwahi kuteua kampuni yenye utaalamu wa majengo yenye lengo na madhumuni ya kutafuta majengo ya ghorofa yaliyokuwa hayajakidhi viwango pia ilibaini kuwa kati ya majengo 100 kati ya hayo 67 hayakustahili watu kuyatumia.

Ugunduzi huo ulienda mbali zaidi kuwa chanzo cha matatizo hayo ni rushwa kwa wakaguzi wa majengo na mamlaka zingine zinazoshughulika na ujenzi mfano Bodi ya Wakandarasi (CRB),

Bodi ya Wahandisi Nchini (ERB) ni tatizo kubwa kama zingefuata maadili ya kazi zao tusingekuwa na matatizo ya majengo yetu kuporomoka mara kwa mara.

Uchunguzi wote huu kama serikali kuanzia awamu ya nne ya Mzee Jakaya Kikwete, John Magufuli na Mama Samia
Suluhu Hassan, zingechukua hatua kali kama zilivyoshauriwa na hizo tume mbili basi ndiyo ingekuwa mwaarubaini wa majengo kuporomoka.

Morningstar Post tutaendelea au kuikubusha serikali majengo yaliyopendekezwa kuvunjwa au kufanyiwa marekebisho ili kupunguza vifo vinavyotokea kwa sababu ya wala rushwa wachache MUNGU IBARIKI TANZANIA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *