
KAMISHINA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo l Septemba 05, 2024 wamekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Taifa wa jumuiya hiyo Stephen Lusinde. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa TRA Dar es Salaam ambapo wamejadili mambo mbalimbali yahusuyo kodi na wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wemesema wapo tayari kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.