





Wataalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi (NaPA) Kitaifa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakishiriki katika kikao cha pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) chenye lengo la kuweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya kusajili Anwani za Makazi katika Hifadhi za Taifa ili kuboresha shughuli za utalii.
Kijao hicho kimefanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TANAPA, Arusha tarehe 27 Agosti 2024