Na Mwandishi Wetu WHMTH, Ruvuma

SERIKALI imemtaka Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wakandarasi wanaopewa kazi ya kujenga minara ya mawasiliano wanasimamiwa ipasavyo kufunga vifaa vyenye nguvu ya usikivu kwenye maeneo ya mipakani ili Taifa liweze kuwa salama pasipo kutegemea nchi jirani.

Agizo hilo la Serikali limetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprica Mahundi tarehe 04 Juni 2024, wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maposeni na Mdundualo watakaonufaika na ujenzi wa minara miwili ya mawasiliano katika maeneo hayo.

Mhandisi Maryprisca amesema minara hiyo inajengwa ili kuboresha huduma za mawasiliano kwa wananchi na kusema kuwa hakuna sababu ya kutumia mawasiliano ya nchi jirani kama Serikali ya awamu ya sita imewawezesha.

Kwa upande wake Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Zablon Magabula amesema amepokea maagizo hayo na shirika linakusudia kujenga minara nane mkoani Ruvuma itakayounganishwa na mkongo wa taifa ili kutoa huduma bora za kijamii likitambua kwamba mawasiliano yana mchango mkubwa kiuchumi na kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *