WAENDESHA  pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda kwenye kijiwe cha FMJ mtaa wa Kisiwani kata ya Buguruni mkoani Dar es Salaam wamempongeza  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi  Hadinan  Karata kwa mafunzo aliyowapatia.

Wakiongea na Morningstarpost kwa njia ya simu madereva hao walisema Machi  29 mwaka huu, walipatiwa mafunzo mbalimbali yakiwemo ya usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima na  namna ya kugundua mapema viashiria vya uhalifu kwa wezi wa pikipiki na wanaowapora abiria wao.

Kwenye mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na madereva wapatao 13 na baadhi ya abiria Mkaguzi huyo wa Polisi ambaye pia ni Askari Polisi wa Kata wa Buguruni aliwashauri waendesha bodaboda kusajili kikundi ili watambulike na pia wanaweza kupata mikopo mbalimbali kwenye taasisi za fedha.

Kwa upande wake Bw. Hadinani alipoulizwa na tovuti ya Morningstarpost alisema ni kweli amewapa mafunzo hayo kama njia ya kupunguza uhalifu na kuwaongezea weledi vijana hao na ameahidi kupita kwenye vijiwe vyote vya pikipiki vilivyopo kwenye kata yake kutoa elimu akishirikiana na viongozi wa serikali kwenye maeneo yao.

Taarifa hii imeripotiwa na Emmanuel  Lyimo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *