. Ni kwa ajili ya kugharamia mradi hewa wa maji
. Nyaraka feki zadaiwa kutumika kufanikisha mpango huo
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CRDB moja ya benki kubwa na maarufu hapa nchini inatuhumiwa kutoa mkopo hewa ambao nyaraka za bandia (Feki) ziliwasilishwa kwenye tawi lake la Mbezi Beach na Mamilioni ya fedha yalichotwa, Morning Star ina ripoti.
Katika sakata hilo benki hiyo ilitoa Mamilioni ya fedha kwa kampuni moja inayojihusisha na miradi ya maji na kufanikiwa kuchota Mamilioni ya fedha kutoka kwenye tawi hilo la benki.
Mtoa taarifa wetu alisema kwamba, kampuni hiyo ya Bigday Company Ltd inayomilikiwa na familia moja yenye ofisi Mbezi Beach, Makao Makuu Jijini, Dar es Salaam ilifanikiwa kuchukua kiasi cha Shilingi Milioni 830,614,083.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa, kampuni hiyo, Bigday Company Ltd iliwasilisha nyaraka feki kuwa imepata tenda Mkoani Ruvuma katika taasisi ya Serikali RUWASA yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2, 231,499,756,47 na kufanikiwa kupewa fedha hizo kupitia tawi la Mbezi Beach kwa mfumo wa “Discount credit “ kama fedha za awali kuendesha mradi huo feki uliopo Mkoani Ruvuma.
Hata hivyo, mtoa taarifa wetu alisema kwamba (sio chombo hiki) walipokutana na ndugu hao wawili, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bigday Company ltd (Jina linahifadhiwa ) alikiri kwamba tatizo hilo lilikuwepo, lakini tayari limerekebishwa.
Morning Star ilifanikiwa kupata nakala za nyaraka hizo zilizotumika katika sakata hilo ambapo fedha hizo ziliombwa Tarehe 21/06/2023 na 14/07/2023 fedha zillingia kwenye hiyo ya kampuni ya Bigday Company Ltd.
Itaendelea.