Mkurugenzi Mtendaji wa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji akipokea tuzo ya pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa Itiji, Halmashauri ya jiji la Mbeya Augustino Kansapa,   ofisini kwake Novemba 11, mwaka huu hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali Mwandishi wetu, Mbeya Wananchi wa Itiji jijini Mbeya wamezungumzia furaha yao na kuridhishwa na utaratibu wa sasa wa utoaji huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.  Wananchi hao wameshuhudia maboresho makubwa kuanzia mapokezi hadi mwananchi anapopatiwa matibabu, ambapo viongozi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali na kuonyesha kutokua na malalamiko kama ilivyokuwa awali. Akizungumza wakati wa kutoa tuzo hiyo Ndg. Augustino Kansapa, Mwenyekiti wa Mtaa wa Itiji ameeleza kuwa kwa sasa wananchi wametambua mchango mkubwa unaotolewa na hospitali kupitia huduma mkoba ambapo wananchi wamekuwa wakizipokea bila malipo na wengi wao wameshukuru kwa kusaidiwa na hospitali katika gharama za matibabu, ambapo wameweza kurejea kwenye afya njema na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo. “Katika kipindi hiki, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya imefanikiwa kupunguza malalamiko ya gharama za matibabu. Wananchi hawalalamiki tena kuhusu hilo kutokana na huduma nzuri wanazozipata katika kuboresha huduma za afya ndani ya jamii, hivyo kwa mapendekezo yao wameamua kuipatia hospitali tuzo kama alama ishara ya kutambua mchango wenu una kuongeza morali kwa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na moyo”.- Kansapa Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, ameelezea shukrani zake kwa tuzo hiyo nakusema kuwa hospitali inathamini sana tuzo hii kutoka kwa wananchi wa Itiji na ishara tosha kwamba juhudi za Serikali za kuboresha huduma za afya zinatambuliwa na wananchi wenyewe na kueleza kuwa watahakikisha kuendelea kuimarisha huduma ili kuhakikisha afya ya kila mwananchi inalindwa na kuimarishwa.” “sisi kama hospitali ya kanda tunatoa huduma kwa watu wengi lakini kutokana na kitendo hichi mlichokifanya ninyi viongozi na wananchi wa Ititji ni kitu ambacho ni cha kipekee ni wachache sana wanaeza kusema ngoja niende kuwashukuru au kuwapongeza kwa zile jitihada zinazofanywa, kwa hiyo kitendo hiki kinazidi kutitia moyo, kutuimarisha zaidi na kutupa deni la kuendelea tutoa huduma bora kwa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini.” – Dkt Mbwanji Kwa upande mwingine Serikali ya Mtaa wa Itiji – Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetoa cheti cha shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, kwa Uongozi wake bora katika kuimarisha huduma za afya na kuleta maendeleo yanayotokana na afya bora kwa wananchi wa Itiji. Serikali ya Mtaa wa Itiji pia imeahidi kuendelea kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na kutoa ushirikiano wa karibu kwa ajili ya maendeleo ya afya ya wananchi wote

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji akiwa na Augustino Kandapa (kushoto)  na viongozi wengine wa hosptali hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *