Na MWANDISHI WETU

KOCHA wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amewachimba mkwara mzito mastaa wake akiwaeleza anataka waendelee kupambana zaidi hasa katika michezo ya ugenini na kuachana na dhana ya kujitoa tu wakati wanapokuwa nyumbani. Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC), kikosi hicho cha Malale kinashika nafasi ya sita, ikiwa na pointi 14, ikishinda mechi nne, sare mbili na kupoteza mitatu. Akizungumzia hali ya timu yake, Malale amesema msimu huu 2023/24 umekuwa mgumu kwa kila klabu, hivyo jitihada zinahitajika kwa ajili ya kuendana na ushindani. “Ligi imekuwa ngumu kwa sababu hujui ni wapi utadondosha pointi, nimekaa na wachezaji na kuwataka kupambana kwa kadri ya uwezo wao bila ya kujali kwani ugenini pamekuwa pagumu zaidi kutokana na kila timu kuhitaji kushinda nyumbani,” amesema. Mzanzibari ameongeza kuwa baada ya ushindi wa mwisho katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar walioshinda mabao 2-1,  nguvu wanazielekeza ugenini tena wakati watakapoumana na Geita Gold kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyankumbu mjini Geita, Novemba 22. “Ni mchezo wa mtego kwa sababu siku zote unapokuwa ugenini ni lazima ujiandae kwa maana ya kiakili na kimwili na hii ni kutokana na kila timu inapigania kupata ushindi hivyo sio rahisi lakini tutaonyesha ubora tulionao,” amesema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *