Na Mwandishi

TANZANIA imeingia kwenye vipengele vitano vya kuwania Tuzo za Soka ya Wanawake Afrika kwa mwaka 2022-2023 ambazo zitatolewa Desemba 11 mwaka huu Jijini Marrakech nchini Morocco.

Katika vipengele hivyo, JKT Queens ambao ni mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati watawania tuzo nne ambazo ni Kipa Bora wa Mwaka kupitia kwa Najiat Abass, Mchezaji Bora Chipukizi kupitia kwa Winifreda Gerald na Kocha Bora wa Mwaka kupitia kwa Esther Chabruma.

JKT Queens, yenyewe ambayo mwishoni mwa wiki ilimaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Ivory Coast itawania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka, huku timu ya taifa ya Tanzania, Twiga Stars ikiwania Tuzo ya Timu Bora ya Taifa ya Mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *