Rangi hizi zinadaiwa kuwa zinawakilisha ushogo ambao nchini tanzania haukubaliki.

Na Mwandishi Wetu

Kampuni moja inayojishughulisha na huduma  ya mikopo kwa wafanyabiashara (jina tunalihifadhi kwa sasa), iliyoko Temeke jijini Dar es Salaam, imeingia kwenye kashfa ya ushoga.

Kampuni hiyo,  wafanyakazi wake wawili wanajihusisha na vitendo vya ushoga, Morningstar Post imebaini.

Akiongea na Morningstar Post ofisini kwake Temeke, Mkurugenzi wa kampuni hiyo alithibitisha kwamba yeye anamjua mmoja wa wafanyakazi wake ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa kuwa ni shoga.

Alisema amekuwa akilalamikiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa wanapokuwa wanatembelea wateja wao kufuatilia madeni wamekuwa wakizomewa na watu kwa kuwa na shoga huyo, hivyo anamtafutia njia ya kumfukuza kazi shoga huyo.

Aliongeza kuwa shoga huyo kwa sasa amekwenda likizo ya kusoma anafikiria akimaliza likizo yake hatomrudisha tena kazini.

Hata hivyo, chanzo cha habari hizi cha kuaminika kinadai kampuni hiyo ina vijana wawili ambao ni mashoga ambao ni wapenzi wakubwa wa mkurugenzi wao amekuwa akisafiri nao kwenda Uganda na zanzibar kikazi mara kwa mara.

Morningstar Post inaendelea kuchunguza na kufuatilia nyendo za kampuni hiyo na wafanyakazi wake baada ya kufanya mahojiano na wahusika itaweka wazi majina yote ya watu wanaohusika na vitendo vya ushoga kwenye kampuni hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *