Na Jones Mwangonda

Zabuni za kutengeneza na kusambaza T-shirt na kofia za Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Serikali ya Mtaa TALGWU, zimelalamikiwa kwa kuweka kiwango kikubwa cha gharama ya kuomba zabuni hizo.

Baadhi ya wazabuni waliozungumza na Morningstar Post, wamemtupia lawama Mwenyekiti wa TALGWU  Bw. Tumaini Nyamhokya kwani ndio ambaye amehusika na kushindwa kusimamia suala hilo kwa kuwa ana kofia mbili za madaraka.

Kwa mujibu wa Tangazo lililochapishwa katika gazeti la Mwananchi Septembe mosi, mwaka huu linaonesha kuwa zabuni hizo namba TALG/PROC/0031/2023 zinaonesha kuwa gharama ya kuomba kitabu cha zabuni ya kutengeneza T-shirt 95,000 ni sh500,000 wakati mwaka jana ilikuwa sh100,000.

Kwa zabuni namba TALG/PROC/0032/2023 kwa ajili ya kuomba kutengeneza na kusambaza kofia 95,000 mzambuni anatakiwa kulipa sh300,000.

Hata hivyo wazabuni wanahoji kwa nini gharama hizo zimepanda mara tano ya mwaka jana ambayo ilikuwa sh100,000 na kumtuhumu mwenyekiti kuwa anafanya hivyo kuweka mazingira ya kuweka watu wake.

Wakizungumza kwa masharti ya kutokutajwa majina yao wazabuni hao wamesema kuwa mwenyekiti ndio alipaswa kusimamia suala hilo kwa kuwa ana kofia mbili kubwa za madaraka hivyo hakuna wa kumlalamikia.

Bw. Nyamuhoka ametupiwa lawama hizo kuwa  amabeba kofia mbili za madaraka TALWGU na TUCTA hivyo kuwa na mgongano wa maslahi katika kusimamia masuala ya haki.

Wazabuni wamemuomba Mweshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwanachama TALGWU kuingilia kati suala hilo.

Walisema kuwa Bw. Nyamhokya amekuwa akivunja bodi za zabuni mara kwa mara mwaka juzi alivunja bodi hiyo na mwaka jana pia alivyunja bodi hiyo ya zabuni na kuchagua bodi mpya.

Waliongeza kuwa ndio maana TAKUKURU wamekuwa wakiingilia kazi zabuni hizi mara kwa mara na hata hivyo kesi nyingi zinasubiliwa kwenda mahakamani.

Akizungumza na Morningstar Post kwa njia ya simu kutoka Morogoro, Bw. Nyamhokya alisema kuwa bei za zabuni ziliamuliwa na bodi ya zabuni.

Alisema kuwa wazabuni wanaoshindwa kulipa gharama ya kuomba zabuni hizo ni wazi kuwa hawawezi kufanya  kazi hiyo.

Hata hivyo hakuweza kueleza kwa undani kuwa kigezo cha kulipa gharama ya zabuni ndio kigezo pekee cha kushinda zabuni hizo.

Bw. Tumaini Nyamhokya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *