Na Alice Hernandez,

Dhihaka ni mbinu ya ghiliba inayotaka kuwafanya watu watilie shaka akili zao timamu au uwezo wao wa kuona ukweli.

Wale wanaoitumia mara nyingi hufanya hivyo makusudi ili kupata kitu.

“Ni tabia ya kibinadamu sana. Ingawa kuna nyakati ambapo tunaweza “kudhihaki” na hatujui, “Dkt. Cortney S. Warren, mwanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Harvard anasema.

Hatari ya mbinu hii ni kwamba ni vigumu kutambua kwamba inatumika kwako.

Inakuwaje?

Mojawapo ya mambo muhimu ni kutambua ikiwa mtu anaposema jambo kwako inakufanya uhisi kutojiamini au kukosa raha, “ni kama unajihoji mwenyewe,” anaeleza Warren, mwandishi wa Letting Go of Your Ex: Skills to Heal the Pain of a Breakup and and Overcome Love Addiction”, 2023).

Anapendekeza kutoendelea mtu anaposema kitu kibaya ama kauli ambayo ni “hatari” ambayo inaweza kutufanya tukose raha na kufikiria kuhusu maoni hayo ambayo yanatusumbua.

Kwa njia hii, jaribu kutathmini maeneo gani unaweza kujibu ama kufanyia kazi.

Njia Warren anaifupisha katika hatua 3: ufahamu, tathimini, na kuchukua hatua.

Mtaalamu huyo anasema lengo, ni kujijua na kujenga kujistahi kwa nguvu ili kukabiliana na hali ya kudhihakiwa.

“Una mtazamo wako, hisia zako, uzoefu wako, historia yako. Kutoka mahali hapo lazima uamini kushughulikia chochote kwa heshima lakini pia kwa mipaka, “anasema Warren.

Lakini kwa kuwa njia hiyo wakati mwingine si rahisi sana, BBC tulizungumza na mwanasaikolojia kuhusu misemo au kauli zenye sumu ‘mbaya’ ambazo zinaweza kujitokeza katika mazungumzo ama majadiliano na jinsi ya kujibu.

  1. “Wewe ni kichaa / Kidogo tu ‘unapaniki, Unaudhika kirahisi’.”

Ikiwa mtu atakuambia kauli hizi, kimsingi anakwambia kuwa huna mawazo ama hoja yenye ukweli.

Wanapokuambia kuwa wewe ‘ni rahisi kuudhika, ndiyo, inaweza kuwa kwamba uko katika wakati ambapo unahisi hisia zaidi. Lakini hiyo ni sawa.

Hakuna kauli inayosaidia kati ya hizi kwa sababu mzungumzaji kimsingi anajaribu kuondoa ukosoaji wowote unaofaa, mahitaji, au hisia ulizo nazo kwa wakati huo na hupuuza wasiwasi wowote ulio nao kama njia ya kuakisi kuwa una hisia nyingi, hata kama kuna ukweli fulani kwake.

Jibu moja unaloweza kumjibu:

“Unaweza kudhani najiweka juu au niko juu kwa sasa. Lakini huu ndio ukweli wangu hivi sasa. Hivi ndivyo ninavyohisi. Hiki ndicho ninachoamini na hiki ndicho ninachokiona.”

“Siko tayari kujadili hisia zangu. Nitakusikiliza, lakini natumaini utaheshimu hilo. Huu ni uzoefu wangu hivi sasa.”

Mtaalamu anatoa ushauri wa ziada kuhusu kauli ama maneno haya ya kuudhi ama yenye sumu. Ikiwa unapitia hisia kali sana, ni vizuri tu kusitisha mjadala ama mazungumzo na kusema, “Nitachukua dakika moja kupumua/kupumzika na kukuambia nini kinanisumbua.”

  1. “Nilikuwa natania tu”

Msemo huu wenye sumu kwa kawaida huja baada ya maoni ambayo kwa kawaida huwa makali sana na yenye uchungu.

Wakati mwingine watu hutoa maoni ya kuhukumu sana, utani mbaya sana na wenye nguvu. Wako makini lakini wanajaribu kueleza maoni hayo kama mzaha. Ni kauli inayoelekea kuwa na kitu cha ubaya ama kukosa utu, Warren anasema.

Jibu moja unaloweza kujibu mtu akitoa kauli hiyo:

Mtaalamu huyo anasema ni muhimu kutambua kwamba maoni hayakuwa ya kuchekesha.

“Huenda ulifikiri huu ulikuwa utani, lakini si utani wa kuchekesha, uliumiza sana hisia zangu.”

  1. “We ndio umesababisha nifanye hivi/Ni kosa lako”

Watu wenye hila hupenda kulaumu wengine kwa uchaguzi wao.

Ili waweze kusema mambo kama vile “Nimekufokea leo kwa sababu umenivuruga” au “Ulichelewa kufika nyumbani kwa hivyo umenifanya nikufokee au nikugombze.”

Lakini kama Warren anavyoeleza, “Huwajibiki kamwe kwa tabia ya mtu mwingine.”

Ndani ya kauli hii pia ni sawa na kumlaumu mtu kwa “kila kitu”, kauli ambayo kwa kawaida ni kali na, kwa hivyo, lazima ichukuliwe kwa umakini.

Daima kuna namna tunavyochangia kuvurugika kwa mahusiano yetu, lakini mtu mmoja hawezi kulaumiwa kwa ukamilifu wa matatizo ya uhusiano.

Jibu moja la kujibu:

Ikiwa wanajaribu kukulaumu kwa walivyoamua, unasema wazi kabisa:

“Tabia yako kwa kweli inaonesha chaguzi zako, sio zangu.”

“Huenda nimefanya mambo ambayo hayakufanya ujisikie vizuri, lakini jinsi ulivyotenda ni wajibu wako, si wangu. Jinsi ulivyofanya ni juu yako, sio mimi.”

Unapolaumiwa kwa tatizo fulani, ni bora kuingilia kati na kusema kitu kama hiki:

“Nina hakika kwamba nina njia ambazo zinafanya kuwe na ugumu kwetu. Ninachukua jukumu langu, lakini siwajibiki kwa yote kwa sababu wewe pia ulikuwa na jukumu ama wajibu katika huu.

  1. “Kama unanipenda kweli, ungeniruhusu kufanya hivi/ ungeniruhusu nifanye hivi?”

Inaweza kuwa jambo lolote kuanzia kutoka kukuomba ulipe bili zote, kuacha kuzungumza na mtu, au kuwa na uhusiano wazi.

Mwisho ni kile ambacho Dk Warren husikia mara nyingi.

“Katika uhusiano wowote kuna kutoa na kupata au kuchukua. Sisi sote tuna mahitaji tofauti na hiyo ni afya, lakini sio ujanja wa kujaribu kukufanya ufanye kitu ambacho hutaki kufanya na kukusukuma kwa kusema haumpendi vya kutosha, hamuendani, au kwa ujumla si mtu sahihi kwakwe.”

Jibu moja linalofaa kujibu:

Mwanasaikolojia anashauri kufikiria kwa uangalifu juu ya mipaka tuliyo nayo na kushikamana nayo.

“Sababu ya kutofanya hivi haihusiani na upendo wangu kwako. Hii ni kwa sababu hivi ndivyo nilivyo na jinsi ninavyotaka kuishi.”

“Sijisikii vizuri kufanya hivyo. Unaweza kuniambia ni kwa sababu nakupenda vya kutosha na siwezi kudhibiti kile unachoniambia, lakini bado, sitafanya kwa sababu sio sawa kwangu.

  1. “Kila mtu anakubaliana nami isipokuwa wewe…”

Hapa mtu anajaribu kuhalalisha mtazamo wake kwamba wewe ni mtu mgumu, mgomvi, akitumia kauli hii kama hoja ambayo watu wengine wenye nguvu katika maisha yako, kama familia yako, wafanyakazi wenzako au mtu yeyote, wanafikiria sawa.

Anafanya unyanyasaji huo uaminike zaidi kwa kujaribu kuwaleta pamoja watu wengine ambao, kwa nadharia, wanafikiri kidhihaka.

Ni njia ambayo wanapaswa kukutenga, kukufanya ujisikie usio na maoni na kutafuta usaidizi huu wa nje ambao kwa kawaida si wa kweli na ni rasilimali isiyo na heshima na uwongo.

Jibu moja la kujibu:

“Ningefurahi ikiwa ungezungumza mwenyewe na sio watu wengine.”

Lengo hapa ni kwa wewe kukumbuka kwamba, kama vile unavyozungumzia ama kujisemea wewe mwenyewe, ndivyo pia mtu inapaswa kuwa hata kwa mtu anayekudhihaki. Na kwamba ikiwa mtu mwingine katika maisha yake ana matatizo na wewe, kama watu wazima, wanaweza kutumia mwanya huo kuzungumzia vibaya.

  1. “Tatizo la kweli hapa ni …”

Hii ni mbinu ya kujaribu kubadilisha mada, kujiondoa kutoka kwenye hoja unayotaka kuongelea.

Ni mbinu ya kusema, “Najua unazungumza kuhusu hili, lakini kwa kweli hoja sio hiyo, hoja ni hii.”

Jibu moja la kujibu:

Muhimu hapa ni kujaribu kubaki kwenye msimamo wako wa tatizo halisi na kutoruhusu liende nje ya mkondo. Usipotoshwe na kugeuzwa kama tiara.

Unaweza kusema kitu kama:

“Unajua niko tayari kuongea chochote, lakini kwa sasa, tatizo nililonalo ni hili.”

“Hilo ni suala tofauti ambalo nitazungumza nawe baadaye ukipenda. Lakini sasa hivi tatizo kuu ni hili”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *